Maisha ni safari ambayo tunaisafiri kila siku. Katika safari tunapata kujifunza mambo mengi sana. Kuna yale ambayo tunapaswa kuyaacha huku mengine tukiwa tuanapaswa kuyakumbatia.
Moja ya kitu ambacho unapaswa kukiacha leo hii ni ile tabia yako ya kununua kila kinachokuja MBELE yako.
Tabia hii si njema sana na inazidi kukupunguzia kipato chako.
Hivyo hakikisha kabla ya kufanya manunuzi yoyote umeyaweka kwenye bajeti yako. Ni kutokea hapo unaweza kununua hicho kitu. Usinunue bila mpango hata kama utaona kitu ambacho umekuwa ukikitafuta kwa muda mrefu bila mafanikio. Kama kwa wakati huo hakipo kwenye mpango wako achana nacho.
Kama unaona bei ya kitu imepunguzwa lakini hakikuwa kwenye bajeti yako achana nacho.
Kumbuka mali bila kalamu, hisha bila habari.