KONA YA SONGA MBELE; Falsafa Mpya Juu Ya Utumiaji Wa Pesa


Habari ya siku ya leo rafiki na ndugu msomaji wa blogu yako ya SONGA MBELE. Karibu sana katika makala haya ya siku hii ya leo tubapoenda kujifunza kitu kizuri sana juu ya pesa.

Kuna watu ambao kila siku wamekuwa wakisema kwamba wao wakishika pesa mkononi mwao basi haikai. Wengine wanasema kwamba hawatulii mpaka pale watakapokuwa wamemaliza kuitumia pesa yote.
Hapo ndipo wanarudi katika hali  ya kawaida na kuendelea na maisha.
Yaani mwingine akipata milioni moja, hatulii mpaka pale ile milioni itakapokuwa kuwa imeisha kabisa.  Rafiki yangu  kama utaendelea na tabia hii kila siku. Sichelewi kusema kwamba unaukaribisha umasikini. Lakini habari njema ni kwamba hizi zote ni tabia na unaweza kuondokana Nazi muda wowote kuanzia sasa.

Sasa kabla hujaondokana na tabia hizi naomba nikuulize swali moja,
Je, u unakumbuka pesa yako ya kwanza kabisa uliifanyia nini?
Kumbuka enzi za utotoni ulipopewa au kupata pesa, uliitumia kufanya kitu gani?

Watu wengi wanakumbuka kwamba pesa yao ya kwanza waliitumia kufanya matumizi ambayo si ya kujenga.
Wapo walioitumia kununua pipi, wengine nguo, wengine kalamu na wengine waliipoteza kwa sababu ya mihemuko. Haya yote ni matumizi ya pesa ya kwanza ambayo hayakuwa mazuri. Na kwa kuwa akili ya mtoto inakuwa katika akili ya kujifunza na kuingiza Maarifa mapya kila siku, basi inapoona inatumia pesa ya kwanza yote inaisha na  matumizi. Basi itajaribu kuendelea kutumia kila pesa inayoingia mfukoni yote. Hii ndio kusema kwamba kama hautabadilika siku hii ya leo na kuanza kuondoa tabia za utotoni basi kila pesa inayoingia utakuwa inaendelea kutumiwa yote mpaka iishe baada ya hapo ndipo utatulia na kuanza kutafuta nyingine. Mzunguko huu utajirudia mara mara kwa mara mpaka siku utakapokuwa umefikia uzee. Huku ukiwa umefanya kazi kubwa sana bila kuwa na mafanikio makubwa sana ya kipesa.

Soma Zaidi; Tabia Tatu Za Pesa

Kwa nini ninaandika kitu hiki tena kwa kujiamini.

Hii ni kutokana na sababu kwamba mwanadamu ni matokeo ya tabia za utotoni. Yaani maisha tunayoishi hapa ni maisha ya utotoni sio vitu vingine ni kuigiza

Hivyo ili kuweza kuondokana na hali hii utapaswa kuvunja moja kwa moja viambatanisho vibovu vya pesa vilivyomo ndani yako. Anza kujenga tabia mpya juu ya pesa.
Kila pesa inapoingia mfukoni mwako, usikimbilie kununua.
Kimbilia kuweka akiba kwanza. Baada ya hapo tumia. Na igundulike akiba hii si ya kula baadae. Bali akiba hii ni ya kuwekeza ili utengeneze pesa zaidi. Itumie akiba kuzalisha pesa zaidi. Itumie akiba hii kujijenga kiuchumi na kuwa wewe Mpya.

1. Kazi ya kufanya leo.
Jiulize pesa yako ya kwanza uliitumia kufanya nini?

2. Je, pesa inapoingia mfukoni mwako sasa unaitumia kufanya nini?

3. Chukua shilingi elfu moja umpe mtoto wako na muulize ataifanyia matumizi gani?
Kama ataandika matumizi yale yale ya nitanunua pipi, biskuti n.k bila kuweka akiba. Hapo ndipo unapaswa kuanzia kumfundisha mtoto wako juu ya somo la pesa.
Mwambie aweke akiba.
Na mwambie juu ya umuhimu wa akiba

Hakikisha hauishii hapo tu, endelea na Somo hili kila siku hata pale utakapokuwa ukimpa pesa ya kwenda shuleni kutumia. Mwambie atoe akiba kwanza na matumizi baadae.

Ulikuwa nami,
Kocha Godius Rweyongeza

Wewe Ni Zaidi ya ulivyo sasa.
Kujiunga na kundi la wasp la HAZINA YETU BONYEZA HAPA
Ndimi
Coach Godius Rweyongeza
godiusrweyongeza1@gmail.com
www.songambeleblog.blogspot.com
Ili kupata kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI  BONYEZA HAPA

Bonyeza hapa ili uweze kupata makala maalumu kila wiki.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X