KONA YA SONGA MBELE; Jinsi Ya Kufanya Kazi Kubwa Kwa Nguvu Kidogo


Habari za siku ya leo Rafiki yangu na ndugu msomaji wa makala kutoka katika blogu hii ya SONGA MBELE, imani yangu leo ni siku njema sana kwako. Na kufika hapa tayari utakuwa umeshafanya makubwa kwenye siku hii ya leo.
Mara nyingi sana watu huwa tunakazana kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja. Huwa tunapenda tufanye vitu vingi sana kwa wakati. 
Hali hii huwa inasababisha kugusa vitu vingi kwa wakati mmoja huku vikiwa na ubora wa chini. Ubora usioridhisha, na ubora usiovutia. 
Ila katika hali ya kawaida akili ya binadamu imewekwa katika mfumo ambao unaweza kufanya jambo moja kwa wakati mmoja. 
Na wewe unahitaji kulijua hili ili liweze kukusaidia kukuza ujuzi mwako na kukufanya wewe uzidi kusonga mbele. Huwezi kufanya kila kitu kwa ubora uleule kwa wakati huo huo, ila unaweza kuchagua vitu vichache vya kufanya kwa wakati na ukavifanikisha. Huwezi kumshawishi kila mtu akubaliane na kile ambacho unafanya ila ukiweza kumbadilisha mtu mmoja kwa wakati inatosha. Basi kwa kujua hilo itatusaidia kuondokana na kupigana na kila kitu badala yake kushughulika na vitu vichache. 
Hivyo leo hii nimekuandalia mambo matatu yatakayokufanya ufanye kazi kubwa sana kwa nguvu kidogo.
1. CHAGUA KITU KIMOJA CHA KUFANYA.
Badala ya kutaka kugusa kila kitu na kujikuta unakifanya bila ya kuwa na ubora, unapaswa kuchagua kitu kimoja ambacho unaweza kukifanya kikachangia kwenye matokeo makubwa sana. 
Najua hapa utaniambia, “unajua mimi Nina kazi nyingi sana, na hivyo siwezi kuziacha”.
Ndio mimi sijakataa kwamba hauna kazi nyingi, ila unapaswa kuchagua kazi moja ambayo unajua ukiifanya itaongeza ubora kwenye Biashara yako.
Jambo moja ambalo unajua ukilifanya litakuongezea umaarufu. 
Chagua jambo moja ambalo kama utalifanya utaongeza kipato mara dufu.
Baada ya hapo, lipe muda wa kutosha kulifanya. Hakikisha unalifanya kwa nguvu zako zote. Na hivyo vingine vinavyochangia kipato au matokeo kidogo vitafuata.
Soma Zaidi Hapa;  Jambo Moja Litakaloinua Biashara Yako Popote Pale Duniani
2. FANYA KAZI BILA KUSIKILIZA KELELE ZA DUNIA.
Kuna kelele nyingi sana. Kuna watu wengi sana wanaongea pale tunapofanya kazi zetu ila kwa kutambua kwamba hatuwezi kumridhisha kila mtu basi tutashughulika na kazi zetu hata kama wengine wanatukatalia katika kile tunachofanya. Hali hii itatufanya tuwe mabingwa na hatimaye kuweza kutufikisha kwenye ushindi kwenye lile tunalolifanya.
Soma Zaidi Hapa;  Nchi Za Ulimwengu Wa Tatu? Au Watu Wa Ulimwengu Wa Tatu? Ipi Sahihi?
3. KUJIFUNZA SANA KATIKA KILE TUNACHOFANYA.
Penda sana kujifunza katika kile unachofanya. Hii itakusaidia na kukufanya uweke juhudi kidogo katika kile unachofanya.
Lakini pia itakuondolea ile hali ya kurudia makosa yale yale ambayo, ungeyarudia ila yalishafanywa na watu wengine. Ondokana na kurudia makosa nunua vitabu sasa ili upate kujifunza zaidi.
Vitabu pia vitakufanya ukae bila kupoteza motisha yako ya kazi.
Nunua sasa kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI. Ili upate kujifunza zaidi.
Kupata kitabu lipa sh.10,000 kwenda 0755848391 jina GODIUS RWEYONGEZA. Baada ya hapo nitumie ujumbe wenye email yako ili nikutumie kitabu.
Utapokea kitabu ndani ya muda mfupi baada ya wewe kutuma pesa.
Karibuni sana.
Wewe Ni Zaidi Ya Ulivyo Sasa,
Wewe Ni Zaidi ya ulivyo sasa.
Kujiunga na kundi la wasp la HAZINA YETU BONYEZA HAPA
Ndimi
Coach Godius Rweyongeza
godiusrweyongeza1@gmail.com
www.songambeleblog.blogspot.com
Ili kupata kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI  tuwasiliane kupitia 0755848391

Bonyeza hapa ili uweze kupata makala maalumu kila wiki.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X