KONA YA SONGA MBELE; Jinsi Ya Kuongeza Ufanisi Kazini


Habari ya siku ya leo Rafiki na ndugu msomaji wa Makala haya ya kona ya songa mbele ambayo hukujia mara moja kwa wiki siku ya jumapili. Wiki hii katika Makala ya kona ya SONGA MBELE tunaenda kuangalia ni kwa jinsi gani tunaweza kuongeza ufanisi katika maeneo ya kazi.

Ikumbukwe kwamba tunapokuwa kazini tunapata fursa ya kukutana na watu mbali mbali. Tunakutana na wasomi waliotoka vyuoni. Tunakutana na watu ambao ni wabunifu. Tunakutana na watu wanaohoji  katika kila kitu.
Lakini pia kuna watu wanajamiiana na kila mtu. Aina hizi zote za watu huwa zina mtazamo tofauti, fikra  tofauti lakini pia zinachukuliana kwa namna tofauti.

Mfano, wasomi wa chuo kikuu, watajiona ndio kila kitu na watawadharau ambao hawajafika chuo kikuu.
Lakini pia watu wabunifu  hawataelewana na watu wanaohoji kila kitu. Na watu wanaojamiiana watakuwa na aina yao ya maisha tofauti na hawa wengine. Lakini wewe ukishawajua watu hawa. Na ukajua kwamba watu wa aina hii wapo basi kinachofuata ni wewe kuwa tofauti ili uweze kufikia mafanikio ya tofauti.

Kwa wiki hii tutaanza kuzungumzia jambo moja ambalo litatufanya tuongeze ufanisi. Wiki zijazo tutazidi kuchimba mbinu nyingine zaidi zitakazotufanya tuongeze ufanisi kazini.

Moja ya jambo unalohitaji ili uweze kufikia ufanisi mkubwa sana kazini ni kutumia SHERIA YA 60-40.

Sheria ya sitini arobaini ni sheria nzuri sana ambayo imetumiwa na watu wengi sana ambao wamefanya kazi kwa ufanisi mkubwa sana kazini.
Soma zaidi; Mambo Manne Yatakayokufanya ung’ae 

Sheria hii ya sitini arobaini inakuhitaji wewe usikilize sana kuliko unavyoongea. Sheria hii inasema kwamba ili uweze kuwaelewa watu lazima uwe makini kuwasikiliza wanachoongea ndipo utawaelewa. Ukiwa na watu ongea kidogo sana yaani asilimia 40% na sikiliza sana kwa asilimia 60%. Ndio maana tunayo masikio mawili na mdomo mmoja. Hii ni ishara tosha kwamba tunapaswa kuongea kidogo na kusikiliza sana.

Ila pia ifahamike kwamba watu wanapenda sana kusikilizwa kuliko wanavyopenda kupewa maelekezo.

Ukipenda sana  kuongea kuliko kusikiliza basi jua kwamba kuna vitu ambavyo utavikosa.

Ukiwa kazini kwako, penda sana kuwasikiliza watu. Waache watu waongee. Waache watu wajieleze. Wewe chambua wanachoongea na kuja na jibu la kwako.

Hiyo inanikumbusha mfalme mmoja ambaye kila alipokuwa akitaka kufanya maamuzi kwenye serikali yake. Basi alikuwa analiita baraza la mawaziri. Baada ya hapo analiambia baraza juu ya maamuzi ambayo angependa kufanya. Baraza linaanza kuumana kwa maneno ya huku na kule. Ndani ya baraza zilikuwa zinatokea pande mbili tofauti. Kila upande unakuwa na maoni yake juu ya jambo hilo lililoletwa na mfalme mezani. Mfalme yeye alikuwa akiwasikiliza tu bila kuongea. Baada ya kila upande wa baraza kutoa hoja za kutosha za kuonesha uko sahihi. Mfalme alikuwa anahairisha kikao bila kutoa maamuzi yoyote. Jambo ambalo  lilikuwa linawaacha mawaziri midomo wazi. Baada ya siku chache wangesikia mfalme kafanya maamuzi juu ya suala hilo.

Soma zaudi; Kama Unapanga Kufanya Jambo Rahisi Maisha Yako Yatakuwa Magumu, Kama Unapanga kufanya Jambo Gumu maisha Yako Yatakuwa Rahisi

Hadithi hii inaoneaha ni kwa jinsi gani tunapaswa kuwa watu wa kusikiliza sana kuliko kuongea

Na wewe anza kuitumia kanuni hii ya sitini arobaini.
Utagundua watu wanasema vitu mbali mbali ambavyo unaweza kuvitumia kufanya maamuzi bora juu ya kazi yako.

Kanuni hii inafanya kazi kwa wanafunzi walio shuleni, waajiriwa, wajasiliamali, wafanyabiashara, wawekezaji, madaktari, walimu, kutaja ila wachache.

Wewe Ni Zaidi ya ulivyo sasa.
Kujiunga na kundi la wasp la HAZINA YETU BONYEZA HAPA
Ndimi
Coach Godius Rweyongeza
godiusrweyongeza1@gmail.com
www.songambeleblog.blogspot.com
Ili kupata kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI  BONYEZA HAPA

Bonyeza hapa ili uweze kupata makala maalumu kila wiki.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X