.
Katika maisha kuna nafasi ya kuchagua vitu mbali mbali vya kufanya. Unaweza kuchagua sehemu unayotaka kwenda. Nani ungependa kukutana naye na kipi ungependa kufanya.
Uchaguzi wa maisha ambayo ungependa kuishi unaufanya mwenyewe.
Uchaguzi wako unaoufanya unatokana na maamuzi. Watu wengi wanaogopa kufanya maamuzi kwa sababu tu wanaogopa matokeo yakayojitokeza. Kila uamuzi unaoufanya unaweza kuja na matokeo chanya au hasi.
Hivyo wewe kama kiongozi lazima uwe tayari kukubali matokeo. Usikubali tu kuona vitu vinatokea. Visababishe. Usikubali tu kuona watu wanashangilia ushindi na wewe kuwa mmoja wapo.
Kosa kubwa ambalo unapaswa kuepuka maishani mwako ni kosa la kuyofanya maamuzi. Jifunze kufanya maamuzi. Kuna maamuzi ambayo utapaswa kuyafanya kwa haraka. Kuna maamuzi utayafanya ili uweze kusonga mbele.
Soma zaidi hapa; Hawa Ndio Kupe Ambao Wananyonya Muda Wako
Usifanye maamuzi kumridhisha mtu. Fanya maamuzi ili kuendana na malengo yako ya sasa.
Leo ni siku ambayo unapaswa kufanya maamuzi Je, utafanya maamuzi gani?
Chukua hagua sasa!