Ndoto KutokaKwa Mama yangu! Ndoto Kutoka Kwa Mwalimu Nyerere


Leo ikiwa ni siku ya Nyerere duniani, basi mengi sana yameandikwa juu ya mwalimu wetu na mengi sana yamesemwa juu ya mwalimu na baba yetu wa taifa. Lakini katika makala ya leo naenda kukuelimisha mambo ya tofauti ambayo ulikuwa bado hujayasoma.

Nikiwa mdogo nilipenda sana kusikiliza hotuba za MWALIMU NYERERE. Kwa hiyo kila siku jioni SAA mbili ilikuwa lazima nisikilize kipindi cha wosia wa baba cha REDIO TANZANIA DARESALAAM kwa sasa TBC taifa.

Nilimwambia mama yangu “kama ningekuwepo kipindi cha Nyerere Mimi ningeiletea nchi yangu ya Tanzania uhuru”. Mama yangu alikaa kimya kidogo afu akanijibu “tunatega masikio kusikia kile utakachofanya, kile utakachokifanya kipindi cha maisha yako ndicho kitakachotuambia kama kweli ungeweza kuiletea nchi yetu Uhuru au la”. Nikiwa mdogo sikumwelewa vizuri sana mama yangu, ila kauli hiyo iliniingia sana kichwani. Tangu hapo nimekuwa nafuatilia ni kwa jinsi gani naweza kuwa msaada mkubwa sana kwa nchi yangu.

Hapo ndipo nilipoamua katika akili yangu kwamba Mimi GODIUS RWEYONGEZA (songambele)  lazima niwe raisi wa Tanzania mwaka 2035. Na hilo limekuwa katika akili yangu kwa siku nyingi sana tangu utotoni. Mpaka leo hii wewe unalisoma hapa kwa mara yako ya kwanza nimekuwa nalo nikilifikria kila siku na kulitafakari na kujifunza zaidi juu ya uongozi.

Lakini pia nikitaka kuhakikisha kwamba nagusa maisha ya watanzania wengi sana basi nikaamua kuanza kushughulika na moja kati ya vitu ambavyo mwalimu NYERERE alikuwa akivisema kama maadui wa nchi hii.
Mwalimu Nyerere alisema maadui wakuu watatu wa nchi yetu ni umaskini, ujinga na maradhi.  Sasa nimeamua kuanza na kuelimisha watu ili wapate kujitambua. Lakini pia nimeamua kuelimisha watu juu ya huyu mjinga anayeitwa umaskini.

Mpaka nitakapokuwa naingia ikulu mwaka 2035 basi umasikini utakuwa umepungua kwa kupitia maisha ya watu nutakayokuwa nimegusa. Mimi mwenyewe nitakuwa tayari bilionea na Niko huru kiuchumi.

Sasa kwa leo ningependa kwa pamoja tujifunze mambo ya muhimu sana ambayo nimekuwa nikijifunza na ninayapenda kutoka kwa mwalimu.

Soma zaidi; Kilichofanywa na Huyu Na Mimi Naweza Kufanya

Je, Wajua Mlango Mmoja Ukifungwa Milango Saba Hufunguliwa

1. Uamninifu
Ukiwa mwaminifu utapendwa sana na watu. Kama ni katika biashara utafanikiwa sana. Maana katika ujasiliamali kuna wakati  unaaaminiwa na kuachiwa pesa na watu ambao wanakuwa wanapata pesa kwa awamu. Ni uaminifu ndio utakaokufanya uzidi kupata watu zaidi.

Katika uongozi uaminifu ni jambo la muhimu sana. Ukikabidhiwa madaraka yoyote yale hata kama ni madogo Fanya kazi kwa uaminifu.
Moja kati ya tabia ambayo nimeigundua kwa watanzania ambao hawana moyo wa kijasiliamali ni tabia ya kutaka kuvuna na kupata pesa nyingi KUTOKA kwenye kampuni au shirika wanalolifanyia kazi. Yaani ukimpa mtu kazi anafikiri atakavyofaidika yeye kwanza kabla ya kuwafikiria wengine. Mtu kama Mwalimu Nyerere hakujifikiria yeye kwanza. Aliwafikria watu wengine kwanza yeye baadae. Jambo hili nalipenda sana.
Na nitalitumia maishani mwangu.

2.  Kusoma na kujifunza kila wakati.
Mwalimu ni moja kati ya viongozi wa Afrika waliokuwa wanafikiria na kuona mbali sana. Alipenda sana kusoma,, alipenda  kujifunza. Jambo hili linazidi kunipa motisha, maana mimi mwenyewe ni mtu ninayependa kujifunza kila siku.

3. Kuandika.
Mwalimu ni moja kati  ya watu ambao wameandika na kuiachia tunu kubwa sana nchi hii. Maandishi ni jambo ambao linadumu kizazi na kizazi na tone moja la wino linawafanya mamilioni ya watu wazidi kufikiria.
Na wewe shika kalamu sasa maana dunia nzima inasubiri kusikia KUTOKA kwako.

Nitaendelea kujifunza na kumfuatilia mwalimu Nyerere kabla na baada ya kuingia ikulu.

Nakutakia siku njema sana Rafiki yangu. Endelea kusoma na kujifunza zaidi.

Wewe Ni Zaidi Ya Ulivyo Sasa,
Wewe Ni Zaidi ya ulivyo sasa.
Kujiunga na kundi la wasp la HAZINA YETU BONYEZA HAPA
Ndimi
Coach Godius Rweyongeza
godiusrweyongeza1@gmail.com
www.songambeleblog.blogspot.com
Ili kupata kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI  tuwasiliane kupitia 0755848391

Bonyeza hapa ili uweze kupata makala maalumu kila wiki.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X