Ni Kweli Watanzania Hatuna Fedha Au Tunachezea Fedha?


Nimerudi tena safuni,
Kueleza ya moyoni,
Langu lengo ni tubuni,
Tupate wetu uhuru.

Naam, naam, naam.
Baada ya kupata kibwagizo cha ushairi huo, sasa karibu sana katika makala ya leo!

Kumekuwa na malalamishi ya watanzania wengi.
Malalamishi ya kwamba hatuna pesa!
Malalamishi ya mshahara hautoshi,
Malalamishi ya magufuri kabana!
Malalamishi ya uongozi mbaya!

Wakati malalamishi hayo yakitokea mambo yafuatayo yanazidi kupamba moto kila kukicha.
Mitoko ya kila wikendi,
Matumizi makubwa zaidi ya mapato
Ununuzi wa magari makubwa ya kifahari
Sherehe za kila namna
Mavazi ya gharama na kuendelea, na kuendelea na kuendelea.

Sasa hapo ndipo huwa najiuliza swali, je, ni kweli watanzania hatuna fedha au tunachezea fedha?

Kipi bora,
Kuvaa mavazi ya milioni na humiliki hisa?
Au
Kumiliki gari la kifahari na unaishi kwenye nyumba ya kupanga?

Kipi bora sasa,
Kuvaa dhahabu za thamani kubwa sana chini mpaka juu huku mtoto akifukuzwa kwa sababu ya karo?
Au
Kutoka outing kila wiki huku familia ikikosa chakula?

Bado nakuuliza, ila naomba univumilie tu na unijibu maswali haya,
Je, ni sahihi kuwatoa marafiki bia kwa round huku ukiwa humiliki hata kipande kidogo cha ardhi katika nchi yako mwenyewe?

Hapa watanzania tunacheza fyongo. Si kweli kwamba watanzania hatuna fedha, ila ni ukweli kwamba

1. TUNA MATUMIZI MAKUBWA ZAIDI YA MAPATO.
Kama wewe unaingiza laki moja na unatumia zaidi ya laki moja, basi jua kwamba umaskini unakuita. Tena unakuita kwa sauti kubwa sana. Kama usipojirekebisha na kuanza kutumia kiasi kidogo zaidi ya matumizi yako, basi miaka kumi ijayo, ndio miaka kumi sitaona ajabu nikisikia kwamba wewe ni omba omba kwenye mitaa ya Dar. Jirekebishe sasa na anza kuwa na matumizi sahihi ya pesa zako.

Soma zaidi;Hii Ndio Biashara Ambayo Kila Mtu Anaweza Kuanzisha

2. HATUTENGI FEDHA KWENYE MAFUNGU MUHIMU.
Fedha inayoingia kwenye mfuko wako unapaswa kuhakikisha kwamba unaitenga na kuiweka katika mafungu matano muhimu.
Mafungu hayo ni,
Fungu la sadaka 10%
Fungu la uwekezaji 20%
Fungu matumizi ya lazima 40%
Fungu la matumizi yasiyo ya lazima (dharura) 10%
Fungu la akiba 10%

Je, unafanya hivyo. Kama hufanyi hivyo jua kwamba unajichimbia kaburi lako wewe mwenyewe. Chukua hatua sasa, muda ni sasa. Usingoje kesho.
Kafungue akaunti hizo benki sasa. Baada ya hapo anza kuweka kila sehemu ya kipato chako kwenye mafungu hayo matano muhimu.

3. HATUNA BAJETI.
Hakuna mtu ambaye huwa anapanga kushindwa, ila huwa tunashindwa kupanga. Kama huwezi kukaa na kupanga bajeti yako, basi jua kwamba unapanga kushindwa.
Kuwa maskini hakukuhitaji kupanga,
Kuwa maskini hakuhitaji malengo,
Kuwa maskini kunakuhitaji usiwe na bajeti ya pesa yako. Badilika sasa, kuwa na akili ya mamilionea kuanzia leo. Hakikisha kila senti inayoingia katika mfuko wako unajua iko wapi na inaenda kufanya nini.

Soma zaidi;  Nimezaliwa Mshindi; Zaeni Mkaongezeke

4. TUNAPENDA MAFANIKIO YA HARAKA.
Mafaniko ya haraka ni jambo ambalo watu wengi wanalipenda sana. Ukijitokeza  na kuwaambia watu kwamba una jambo ambalo wanaweza kufanya leo kesho wakaamka matajiri basi utapata wafuasi wengi.
Watu hawataki kuwekeza kwenye kufuatilia uwekezaji sahihi, watu hawataki kujua ipi ni Biashara bora ya kufanya na kwa wakati gani! Yaani mtu akisikia, wekeza hapa leo kesho utajirike basi hapo ndipo kwake.
Ukimwambia fuatilia kwanza, basi hapo mtakosana.
Anza kuishi kwa utofauti, jitofautishe mwenyewe usije ukafa.

Soma zaidi; Hivi Ndivyo unaweza Kuwanasa Watanzania Wengi

Wewe Ni Zaidi Ya Ulivyo Sasa,
Wewe Ni Zaidi ya ulivyo sasa.
Kujiunga na kundi la wasp la HAZINA YETU BONYEZA HAPA
Ndimi
Coach Godius Rweyongeza
godiusrweyongeza1@gmail.com
www.songambeleblog.blogspot.com
Ili kupata kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI  tuwasiliane kupitia 0755848391

Bonyeza hapa ili uweze kupata makala maalumu kila wiki.


One response to “Ni Kweli Watanzania Hatuna Fedha Au Tunachezea Fedha?”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X