Habari,
Kumekuwa na maoni kwa watu mbali mbali, viongozi wa serikali, taasisi, wasomi pamoja na watu kutoka katika nyanja mbali mbali za kimaisha. Maoni haya yamekuwa ni juu ya maendeleo ya watanzania kwenye jumuiya ya afrika mashariki. Jumuiya hii ni nzuri na bora sana, kwa maana inatoa fursa ya nzuri kwa watanzania kuwekeza na kuwa wigo mpana sana wa masoko kwa bidhaa zetu. Hata hivyo bado hawaichangamkii fursa hii. Jambo hili limekuwa likinipa maswali mengi sana. Binafsi nilijua labda tu, watanzania hawatako kuchangamkia vitu kama kusoma kwa sababu wameaminishwa kwamba ukitaka kumficha mwafrika kitu kiandike katika kitabu. Lakini pia labda nikawa nafikiria kwamba labda watanzania hawatako tayari kujihusisha na ujasiliamali kwa sababu unahitaji kutumia nguvu, akili na muda mwingi hasa pale anapokuwa anaanza.
Kumbe watanzania hata hawataki kushiriki katika fursa za kielimu zinazotolewa ndani na nje ya nchi kwenye vyuo vikuu mbali mbali.
Kumbe watanzamia hata hawataki kushiriki katika vitu vibavyojenga jamii, hasa mazingira yaliyotuzunguka.
Sasa hapa sababu ni nini?
Yaani tushindwe kusoma vitabu,
Tushindwe katika kutunza muda kwa kisingizio cha cha hakuna haraka barani afrika,
Tushindwe ujasiliamali,
Na tushindwe katika fursa za kusomeshwa, tena buree!
Hii ndio inazidi kunipa picha ya kwa nini hata watanzania hawahudhurii katika semina za bure.
Katika kuzidi kufuatilia ndipo nimekuja sababu mbili (02) zinazowafanya watanzania wazidi kurudi nyuma katika suala zima la mafanikio.
1. UTHUBUTU.
Yaani hata kama mtu angekua ananiambia kwamba andika kitu kimoja tu kitakachobeba ujumbe mzima kwenye makala hii basi ningeandika neno KUTHUBUTU nikamaliza.
watanzania ni wakali wa kudhubutu kwa kupost na kuwa updated katika mambo ambayo si mazuri. Lakini si wepesi wa kuthubutu katika kusoma, kutafuta Maarifa na kuwekeza. Laiti kama hali hii itajiendeleza, watanzania wengi watazidi kupigika na pengine kufikia hatua ambayo labda wataamka na kuanza kuchukua hatua za kubadilisha maisha yao.
Sasa ebu wewe anza kuchukua hatua siku hii ya leo. Usiishie tu kulalamika kwamba serikali haitujali. Usiishie kulalamika maisha magumu.
Ishia kuziona fursa na kuzitumia. Yaani mimi katika akili yangu sioni haja ya wewe kuendelea kulalamika huku sasa ni mwaka wa kumi kwamba maisha ni magumu. Mwaka jana ulisema maisha ni magumu, mwaka huu nao unasema maisha magumu na mwaka kesho bado ulalamike maisha magumu.
Chukua hatua juu ya maisha yako.
Kwa maoni yangu malalmishi yote inayotupiwa serikali chanzo chake ni wewe.
Malalamishi ya madini yanayopotea chanzo chake ni wewe.
Malalamishi ya wanyamapori wanaozidi kuchukuliwa na kupotea chanzo chake ni wewe.
Yaani huwezi kuniambia suala la wazungu nikakuelewa hata kidogo.
Kama wazungu walikuja miaka ile na kututawala, na sasa bado wapo? Najua utasema ndio. Tena utaendelea kusema hivi huyu Godius Rweyongeza hajui kwamba kuna ukoloni mamboleo.
Hahahah! Ukoloni mambo leo!!!!
Ngoja nikuulize, wazungu ndio wanakuzuia wewe kuweka akiba??
Achana na hilo, ebu sasa jibu hili. Kwani wazungu ndio wamekuambia kwamba uamini wao ndio wawekezaji pekee!
Wako wamekuambia kwamba usiitumie ardhi hiyo iliyopembeni mwaka mpaka pale watakapokuwa wamekuja kuwekeza ili wewe uanze kulalamika kwamba ardhi yetu imechukuliwa?
Kama hautachukua hatua leo hii kuhakikisha kwamba umebadiliaha kuwa yanayoonekana utaiahia tu kulalamika miaka nenda miaka rudi. Maisha ni wajibu wako. Timiza wajibu wako leo hii.
Soma zaidi; Kona Ya Songa Mbele; Zaeni Mkaongezeke
2. ELIMU
Hapa katika suala la elimu naenda kulizungumzia katika mitazamo miwili.
Kuna watanzania hawataki kuchukua hatua kwa kisingizio cha kwamba hivi vitu vinafanywa na wasomi. Na wasomi wenyewe hawachukui hatua. Nao wanasingizia kwamba hivi vitu au kazi hizi za watu wasiosoma yaani kunakuwa kutupiana mpira juu ya kutupiana mpira.
Sasa ngoja niongee na wewe! Usiogope! Haijalishi elimu yako, wala kipato. Kama unaona fursa ya kufanyia kazi, ifanye.
Hakikisha kwamba unatafuta Maarifa sahihi kwenye kile unachofanya. Usiishie kusema ni vigumu..
Kila kitu kama utachukua hatua. Soma Kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI upate pa kuanzia
Watanzania chukueni hatua leo hii, huu utagemezi tunapaswa kuuondoa. ili Tanzania iweze kuwa dola kubwa duniani wewe unapaswa kuwa mkubwa. Hatuwezi kuwa dola kubwa lenye watu wadogo, wasiojiamini na wasiochukua hatua. Laiti kama hutachukua hatua siku hii ya leo. Narudia leo hii. My friend, malalamishi yako yataendelea kuwepo mpaka siku unaaingia kaburini.
Kwa leo naishia hapo tu!
Ulikuwa nami,
Kocha Godius Rweyongeza.