Habari za siku ya leo rafiki yangu. Leo ni siku njema sana katika dunia hii kuwahi kutokea,
Siku hii ya leo tutaangalia sheria kuu tatu za pesa. Baada ya kuzifahamu sheria hizi zitatusaidia sana sisi kutengeneza utajiri na kuwa watu wakubwa sana hapa duniani. Yaani ikiwa ni pamoja na kufikia Uhuru wa kiuchumi.
Ikumbukwe kwamba pesa kama pesa, zina kanuni zake kama ambavyo vitu vingine vina kanuni zake. Kanuni hizi. Zinafanya kazi uwe Afrika, au sehemu nyingine hapa duniani.
1. Pesa inashuka thamani kila mwaka.
Hakuna pesa ambayo haishuki thamani hapa duniani. Hata ile dola ya kimarekani ambayo watu ndio hufikiri ipo salama, inashuka thamani.
Sasa hii ina msaada gani?
Ukilijua hili maana yake unapaswa kuhakikisha kila mwaka kipato chako kinaongezeka kwa kiasi kikubwa kuliko mfumuko wa bei katika nchi yako. Hivyo kitu cha kwanza unapaswa kufahamu mfumuko wako wa bei katika nchi yako ni kiasi gani? na baada ya hapo ufanyie kazi, kwa kuhakikisha kipato chako kinaongezeka walau mara dufu kila mwaka.
Soma Zaidi; Kona Ya Songambele; Falsafa Mpya Juu Ya Utumiaji Wa Pesa
2. Punguza kiwango cha kulipa kodi
Kama umewahi kufuatilia kila uongozi mpya wa kiserikali ukipita kwa wananchi kuomba kura basi huwa wanahaidi mambo makubwa sana. Utasikia wanasema, tutaleta barabara nzuri, tutaleta hispitali, na huduma nyingine nyingi za kijamii. Sasa swali la kujiuliza hawa pesa wanazitoa wapi?
Kiukweli serikali haizalishi. Maana yake inategemea kodi yangu mimi na wewe hapo. Tukilipa kodi serki inapata pesa za kuendeshea shuguli zake za kila siku. Umeona hapo. Sasa unapaswa kujifunza jinsi ya kulipa kodi kidogo bila kuvunja sheria za serikali. Hii ndio siri kubwa sana, ya wajasiliamali. Na hii ndio siri kubwa sana wanayoitumia watu wanaotaka kuwa huru kipesa. Na wewe itumie hii.
Matajiri ni watu waliojifunza hili na wanalitumia kila siku.
Soma Zaidi; Vitu Nane Vya Kuzingatia Kabla Ya Kuanzisha Biashara
3. Weka akiba.
Ingawa kuna mfumuko wa bei unaotokea kila mwaka. Na ingawa bado kuna kodi unayopaswa kulipa. Hakikisha kwamba unaweka akiba. Akiba hii ije iwe ya wewe kuja kuwekeza kwa siku za mbeleni.
Weka akiba katika senti inayoingia mfukoni mwako.
Hizi ndizo sheria tatu ambazo nilipenda uzifahamu siku hii ya leo. Zinaonekana ni rahisi sana, lakini kama utazitumia vizuri kwa hakika zitakuweka huru.
Soma Zaidi; Fanya Kile Ambacho Wengine Wanaogopa