Habari,
Katika maisha yetu ya kila siku pesa imekuwa ikizungumziwa sana. Pesa imekuwa ikitajwa na watu kutoka katika kila kona. Kila unachogusa ni pesa. Ukitaka kusafiri pesa lazima it itumike. Hata hapa unasoma makala hii kwa sababu kuna pesa umeitumia kununua vocha. Yaani kwa maisha ya sasa suala zima la kuwa na pesa si la jambo ambalo unaweza kulikwepa.
Soma zaidi; Je, Kupenda Pesa Ni Chanzo Cha Maovu?,
Mababu wetu walikuwa na uwezo wa kulikwepa hili. Hii ni kutokana na mfumo wa ubadilishanaji uliokuwa unatumika kwa wakati huo. Kipindi kile ilikuwa rahisi kulima kwenda kubadilishana muhogo kwa viazi au Ndizi.
Mfugaji kwake angeweza kwenda na ng’ombe wake saba akabadilishana na magunia ya mahindi kwa mkulima na maisha yangeendelea vizuri tu bila kuharibu kitu chochote.
Sasa kwa kuwa pesa imekuwa muhimu sana katika ulimwengu wa leo. Basi kuzifahamu tabia za pesa ni jambo muhimu sana.
Hizi hapa ni tabia Tatu muhimu kuhusu pesa.
1. Pesa ni muhimu.
Moja kati ya kauli maarufi sana kutoka kwa watu ni kauli za “fulani ana pesa na Mimi sina ila hanizidi kitu chochote”. Mwingine utasikia akisema “matajiri hawaishi kwa raha”.
Kauli kama hizi ingawa zinaweza kuwa na ukweli kwa baadhi ya watu lakini kwa asilimia kubwa si kweli.
Usiishie kujifariji tu kwamba Mimi sina pesa na ninaishi maisha mazuri na sina tofauti na fulani.
Pesa ni muhimu sana kwako. Itafute ili ikusaidie.
2. Pesa ni mtumwa mzuri sana.
Pesa ipo ili ikutumikie kama mtumwa. Kama wewe utakuwa mtumwa wa pesa basi jua kwamba utahangaika sana.
Jua ni wapi unapaswa kuiwekeza ili pesa izidi kukuongezea pesa hata kama umelala.
Soma zaidi; Mambo Manne Kuhusu Pesa Unayopaswa Kuyafahamu
3. Pesa ni ipo ili izunguke
Pesa haipo ili itunzwe na kufichwa ili isionekane. Pesa inapaswa kuwekwa katika mzunguko kila wakati.
Kumbuka kama hutaiweka katika mzunguko pesa basi jua kwamba utaendelea kushilia makaratasi ambayo yanashuka thamani kila siku.