Habari za siku ya leo Rafiki yangu na ndugu msomaji wa blogu ya songambele.
Imani yangu leo ni siku njema sana kwako. Hakika tarehe 04 ya mwezi 10 21017 ni siku ambayo haijawahi kujitokeza maishani? Tafuta kalenda zote hutakuja kuiona. Lakini hata kama bado utaambiwa uishi miaka mingi sana hapa duniani basi jua kwamba hutakuja kukutana na siku iitwayo tarehe 04 oktoba 2107. Ishi leo. Fanya kila kitu leo. Kamwe usihairishe wala usikubali kitu chochote kile kikurudishe nyuma. Hakikisha leo hii unafanya kazi bila kisingizio.
Hivi ulishawahi kujiuliza kwamba maishani kuna takataka ambazo zimetuzunguka ila kwa kuwa maisha yetu yako bize sana hata huwa hatupati muda wa kuziangalia na kuhakikisha kwamba tumezichoma takataka hizi?
Najua hapa utajiuliza mara mbili tatu. Pengine utashangaa kuona wewe ambaye huwa unafagia kila siku kiwanja cha nyumba yako inakuwaje mtu anakwambia kwamba wewe hujafagia takataka zilizokuzunguka na kuzichoma?
Kiukweli ninaposema kwamba kuna takataka ninamaanisha. Takataka nyingi sana zimetunguka na hatutaki kuzichoma.
Kwani takataka ni nini? Kamusi ya kiswahili sanifu ya Tanzania (TUKI)inaelezea takataka kama “vitu ambavyo havifai kwa matumizi na hupaswa kutupwa”.
Viti hivi ni vipi? Je, na Mimi ninavyo?
Basi katika makala ya leo hii twende pamoja ili ujifunze takataka hizi baada ya hapo uzichome na kuziangamiza kabisa
1. Marafiki wabaya
Je, wajua kwamba kuna watu ambao wamekuzunguka ila hujatulia hata kidogo kuhakikisha kwamba watu hawa unapuliza kipenga na kuwasimamisha ili wewe uendelee mbele. Kila siku inakuwa na kelele nyingi sana kutoka kwa marafiki. Wapo wanakuambia huwezi. Wapo wanaokuambia wewe maisha yako yatakuwa mabaya sana. Wengine wanakuambia haiwezekani. Hakika hawa ni takataka. Kama hawataki wewe uzidi kusonga mbele huna haja ya kuendelea kuwakumbatia. Waangushe chini sasa ili wewe uzidi kusonga mbele. Watupe kwenye shimo la taka, na kuwachoma. Ninaposema kuwachoma simaanishi kwamba uue. Ninamaanisha kwamba usiwaruhusu waendelee kuhukumu kazi zako. Usiwaruhusu waendelee kukuvuta na kukurusisha nyuma.
Kazi ya kufanya sasa, angalia ni watu gani ambao ukiwaambiabkwamba Mimi….nitafanya kitu fulani na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa wanakataa. Angalia ni kwa namna gani utaacha kuwashirikisha katika kazi zako.
Kumbuka; kadri watakavyozidi kukwambia kwamba huwezi ndivyo utakavyozidi kutoweza.
Soma zaidi; Nisome Sms 1000 Au kurasa 1000? Kipi Sahihi? Nifanye Kipi?
2. MAWAZO HASI.
Kama unafikiri hasi juu yako basi utavuna ulichopanda. Unahitaji kuwa mtu chanya juu yako. Fikiri chanya. Tenda chanya. Ishi chanya. Kuna vitu ambavyo huwa vinatokea na muda mwingine kutulazimisha kuongea hasi, achana navyo. Usikubali vitu hivi vikurudishe nyuma. Endelea kupigana kwa nguvu zako zote. Hata kama utakutana na matatizo au changamoto. Huu ndio muda wako muafaka wa wewe kuhakikisha kwamba unazitumia changamoto hizo kama nafasi ya kukua.
Fikiri chanya juu yako mambo yote yataenda sawa. Fikiri chanya juu ya Rafiki zako. Fikiri chanya juu ya kila mtu unayekutana naye. Kamwe, usikubali kuendeshwa na maisha katika kufikiri. Usikubali matokeo yanayotokea yakubadilishe mtazamo wako.
3. UOGA.
Moja kati ya vitu ambavyo vinasumbua watu wengi sana ni uoga. Kila nikipokea simu KUTOKA kwa watu utasikia wakikuambia kwamba “mimi unaogopa kusimama mbele ya watu”. Mwingine atakuambia “mimi nikisimama mbele ya watu naanza kutetemeka”. Mara utasikia “yaani mimi unaogopa kuongea, hasa pale ninapokutana na wageni”.
Hakika uoga ni kitu ambacho kinasumbua watu wengi sana. Laiti kama kila mtu angelijua kwamba uoga si kitu. Basi pasingekuwepo na mtu anayeogopa.
Uoga ni hali ya akili ambayo wewe hapo unaitengeneza katika akili yako.
Kama kuna kitu unaogopa kukifanya. Chukua hatua sasa na hakikisha kwamba unaenda mbele zaidi na kukifanya. Hakuna sababu ya kusema unaogopa. Chukua hatua sasa.
Je, kitu gani ulikuwa unaogopa kufanya? Kiandike chini kwenye karatasi. Sasa toka nje na kakifanye sasa. Usirudi kwa sababu ya uoga. Endelea pale utakapojisikia kama unataka kuacha lwe sababu ya uoga jipe muda zaidi wa kukifanya.
Hakika kama utafanya hivi kwa mwezi mmoja basi hali hii ya uoga itapotea. Fanya hivi kwa kila jambo ambalo wewe unaonekana kuliogopa.
Soma zaidi:Jambo Moja Litakaloinua Biashara Yako Popote Duniani
Kwa leo kayafanyie kazi haya. Hakikisha haujiwekei kikwazo chochote cha kutochoma takataka hizi. Chukua hatua sasa. Muda ni sasa, anza sasa, ishi sasa.
Tukutane kileleni