Umuhimu Wa Kilimo Cha Bustani


Habari ya siku hii ya leo rafiki yangu. Kama ilivyo ada kila ijumaa tunapata makala za kilimo ambazo zinajikita katika kutuelimisha juu kilimo bora.

Leo hii tunaenda kuangalia umuhimu wa kilimo cha bustani.
Kilimo cha bustani ni kilimo kinachohusisha kulima eneo dogo sana kwa weredi wa hali ya juu sana. Kilimo cha bustani kinahusisha kulima mboga, matunda, viungo na mapambo mengine. Kilimo hiki kina umuhimu mkubwa sana kwa watu wote hapa duniani.

1. Huwa napenda kuwaambia watu kwamba hakuna siku ambayo itapita bila mtu hapa duniani kutumia zao linalotokana na kilimo cha bustani. Anaweza kuwa amelitumia moja kwa moja au si moja kwa moja, lakini kwa siku wewe lazima utumie zao la kilimo cha bustani.

Hili linaweza kuwa ni tunda, kama Ndizi, embe, nanasi, chungwa, papai, pera kutaja ila macahache. Matunda haya unaweza kuyatumia moja kwa moja au unaweza kuyatumia kupitia vinywaji na vyakula vya viwandani kama sharubati (juisi).
Hivyo hakikisha unachagua kuwa mmoja wa watu wanaotoa walau zao moja kutoka katika kilimo cha bustani ili uweze kukidhi mahitaji makubwa sana ambayo watu wanapenda yatimie.

Soma zaidi; Hizi Ni Sababu Kumi Na Tatu (13) Zitakazokufanya Uingie Kwenye Kilimo Cha Bustani Leo

2. Kilimo cha bustani ni cha kimataifa. Mara nyingi mazao ya kilimo cha bustani ni mazao yanayotumika duniani kote. Hivyo ukilima mazao haya utakuwa na uhakika wa kuuza popote duniani.

3. Lishe. Mazao ya kilimo cha bustani yanashauriwa sana kwa ajili ya kutunza afya za watu. Mazao kama matango, pilipili, vanila na mengine mengi yanashauriwa sana na wataalam kwa ajili kuboresha lishe za watu.

4. Kilimo Cha bustani kinapendezesha mazingira. Ukienda katika mahoteli na katika maeneo mbali mbali nyumbani na mjini. Utakuta maua yamepandwa kupendezesha mazingira. Kumbe na wewe unaweza kuwa miongoni mwa watu wanaosaidia watu kupendeza mazingira kwa kutoa maua mazuri au kwa kushiriki kulima maua maeneo mbali mbali

5. Chanzo cha kipato.
Kilimo cha bustani ni chanzo kizuri cha kipato. Kama wewe unapenda kujiingizia kipato kwa mtaji kidogo sana, sehemu nzuri ya wewe kuanzia ni kwenye kilimo cha bustani.

Kwa leo naomba niishie hapo. Tukutane  wiki ijayo kwenye makala kama haya ya  kilimo

Wewe Ni Zaidi ya ulivyo sasa.
Kujiunga na kundi la wasp la HAZINA YETU BONYEZA HAPA
Ndimi
Coach Godius Rweyongeza
godiusrweyongeza1@gmail.com
www.songambeleblog.blogspot.com
Ili kupata kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI  BONYEZA HAPA

Bonyeza hapa ili uweze kupata makala maalumu kila wiki.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X