Fursa Tano (05) Ambazo Unaweza Kuzifanyia Kazi Katika Kilimo Cha Bustani Leo


Kilimo Cha bustani ni sekta ambayo inakua na kuongezeka wigo wake kila kukicha. Watu wengi sana kwa sasa wamekuwa wakijihusisha na kilimo hiki. Mazao yake sasa yamepata soko kubwa sio tu kwa ndani ya nchi yetu, lakini pia nje ya nchi yetu

Kutokana na hizo fursa zinazozidi kujitokeza, na kutokana na ukweli kwamba watu bado hawajanona ni  kwa jinsi gani unaweza kufadidika na sekta hii. Leo hii nimekuandalia Makala maalum ya jinsi gani unaweza kupata pesa kutola kwenye sekta hii.

1. MBEGU
Wakulima wa katika sekta hii wanahitaji mbegu bora. Leo hii ukiamua uanze kuwafikishia mbegu hizi katika maeneo walipo watashukuru sana, lakink pia watakuwa tayari kukulipa ili wapate huduma yako bora.

2. KEMIKALI NA MBOLEA
Wakulima wanahitaji mbolea ya kupandia mazao pamoja na mbolea ya kukuzia. Mbolea hizi mara nyingi hazipatikani katika maeneo yote hapa nchini. Mbolea hizi zinakutwa sana sana maeneo ya mijini, ingawa bado kuna wauzaji wake wanauza mbolea ambayo hazia viwango. Unaweza kuingia huku ukawahakikishia uwepo wa mbolea hii muda wote watakapoihitaji.

3. KEMIKALI
Wakulima wanahitaji kemikali muhimu sana kwa ajili ya kuua wadudu, na wanyama wanaoshambulia mazao yao ya kilimo cha bustani. Wewe wape uhakika wa kuwaletea kemikali hizo ili wako walime kwa raha.

4. UMEME NA PETROLI
Katika maeneo mengi sana hapa nchini wakulima wengi wanatumia petroli kwa wingi katika kuvuta maji kutoka katika vyanzo vya maji mpaka kwenye mashamba yao. Maeneo machache yanatumia Umeme. Hivyo unaweza kuwaangalia wakulima waliokuzunguka wako wanatumia nini na kuamua kuwaaogezea huduma ya Umeme au petroli karibu.

5. VIFAA
Kuna vifaa ambavyo vinatumika katika kilimo. Vifaa kama jembe, shoka mashine n.k
Unaweza kuwaangalia wakulima wanaokuzunguka na kuamua kuwaletea huduma hiyo karibu.
Asante


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X