Habari ya leo Rafiki yangu.
Kwa siku sasa nimekuwa nashuhudia watu mbalimbali wakishiriki katika kushangilia siku za kuzaliwa.
Watu wamekuwa na utaratibu wa kumumwagia maji mtu ambaye anasheherekea siku yake ya kuzaliwa kwake.
Sijajua utaratibu huu umetokea wapi ila walau ninachojua ni kwamba watu wameupokea na wameukumbatia sana utaratibu huu.
Utaratibu mpaka sasa umekuwa sehemu ya pili ya maisha ya baadhi ya watu. Yaani wanajua wakisikia kwamba mtu fulani anaazimisha miaka kadhaa ya kuzaliwa kwake wanachofanya ni kumvizia popote pale ili amwagiwe maji. Wengine wameenda mbali zaidi kwa kuwapaka watu matope na majivu na baada ya hapo kuwaogesha wahusika.
Sasa sijui utaratibu huu umeletwa na nani, kutoka katika nchi gani? Huyu mtu sijamjua ila kama nikimjua nitampongeza sana.
Nitampongeza kwa sababu kutokana na utaratibu wake aliouleta sisi tunaenda kuibuka na utaratibu mpya wa kumwagia watu maji.
Utaratibu huu mpya ambao sisi tutaibuka nao leo hii ni utaratibu bora sana kuwahi kutokea katika dunia hii na nina hakika kwamba mtu yeyote yule ambaye ataukumbatia utaratibubhuu basi utakuwa wenye manufaa majubwa sana kwake.
Utaratibu huku utaweza kumwinua na kumtoa haoo aipo na kumepeleka hatua ya ziada. Kama ambavyo nimezoea kusema kwamba utaratibu huu utatoa watu KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI.
Utaratibu wenyewe ni kumwagia watuu maji safi. Maji yenyewe ni vitabu.
Badala ya kumumwagia mtu maji siku yake ya kuzaliwa tunaenda kuanzisha utaratibu wa kumwagia watu vitabu siku zao za kuzaliwa. Vitabu ni maji mazuri ambayo kama tutawamwagia watu hatutawaacha tu kama walivyo Bali tutawaachia maarifa. Tutaweza kuwainua kutoka sehemu walipo..
Kuna mtu aliwahi kusema “rafiki Wangu wa kweli ni yule anayenipa kitabu”. Binafsi nakubaliana na usemi huu. Rafiki wa kweli hawezi akawa mtu anayekumwagia maji siku ya kuzaliwa na kuondoka.
Lakini kama atakumamwagia maji safi ambayo ni maji ya Kitabu. Basi huyo ni Rafiki wa kweli.
Kuanzia leo tuanze kumwagiana maji ya vitabu. Badala ya kukaa na kuanza kufikiri ni kwa jinsi ganinunaweza kuwasuprise watu kwa kuwamwagia maji. Kaa fikiri ni Kitabu gani unaweza kumpa mtu siku ya kuzaliwa kwake.
Hizi ndizo surprise ambazo binafsi nazipenda sana..
Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio.
Tukutane kwenye mzunguko wa wanamafanikio