Haya Ndio Mambo Mawili Yanayofanya Watu Wasiwe Na Maisha Bora


Linapokuja suala la kuwa na maisha bora sana watu wengi sana wamesema mambo mengi sana. Wapo wanaosema kwamba wameshindwa kuwa na maisha bora kwa sababu ya mazingira. Wapo wanaosema wameshindwa kuwa na maisha bora kwa sababu wazazi wao hawajawatengenezea mazingira. Wapo wanaosema wao wamezaliwa kuwa hivyo.

Hata hivyo binafsi sijamwona mtu mwenye sababu za maana kati ya hao.

Yaani uniambie mazingira yanakufanya usiwe na maisha bora! Mazingira gani unayataka zaidi ya hayo uliyo nayo sasa. Unahitaji nini ambacho kwa sasa hauna? Dunia hii ni njema sana. Yaani mpaka wewe unazaliwa ilikuwa tayari imeandaa mazingira kiasi cha kutosha. Mpaka hapo hakuna kitu unachokosa. Kila kitu unacho. Ndio maana ukazaliwa katika mtaa huo ulipozaliwa, na wazazi hao! Ndio maana ukasoma shule hiyo uliyosoma, tena ukakutana na watu haoo! Hii yote sio bahati mbaya. Haya yote ni mazingira unayohitaji kufanikiwa na kuwa na maisha bora.
Tatizo sio kwamba mazingira ni mabaya, tatizo hutaki kuona uzuri wa mazingira yako.

Na wewe unaniambia wazazi hawakuniandalia mazingira mazuri. Inaelekea hauko makini na maisha yako. Yaani mpaka umekua, umesoma na kufika  hapo unasema hujaandaliwa mazingira mazuri???
Mazingira gani unahitaji? Au unahitaji ghorofa?? Majua hapa umeschekelea na kusema ndio!!!
Unaendelea kusema kwamba Godi hapa ameanza kunielewa.
Hahahah! Mimi nipo nakushangaa tu! Kila kitu kinachohusiana na mafanikio na maisha bora tayari kipo na kimewekwa ndani yako.

Hizi hapa ni sababu mbili zinazokufanya usiwe na maisha bora.

1. Hauna Ndoto.
Maisha bila ndoto sio maisha. Maisha ambayo hujui unaenda wapi si maisha. Hakikisha kwamba unakuwa ndoto kubwa sana katika maisha yako.

2. Unalenga chini sana.
Ili utoke sifuri mpaka kileleni unahitaji kulenga mbali sana. Usiangalie tu hapa karibu. Ona mbali sana kuanzia sasa.

Ebu chukua hatua sasa ili upate kujifunza ndani ya kundi hili.
Wewe Ni Zaidi ya ulivyo sasa.
Kujiunga na kundi la wasp la HAZINA YETU BONYEZA HAPA
Ndimi
Coach Godius Rweyongeza
godiusrweyongeza1@gmail.com
www.songambeleblog.blogspot.com
Ili kupata kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI  BONYEZA HAPA

Bonyeza hapa ili uweze kupata makala maalumu kila wiki.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X