Haya Ndio Maneno Yanayotumiwa Na Watu Kujifariji Linapokuja Suala La Pesa


Nimegundua kwamba mtu anapokuwa hana kitu anatafuta njia ya kuonesha kwamba yeye yupo sahihi kwa asilimia 100%. Yaani yeye kushindwa kukipata kwake ana kutumia kama nafasi yake kuonekana kwaba yeye ni mtu ambaye yuko sahihi kwa asilimia mia moja.
Mfano unakuta wavulana hawajui kujieleza basi wanachukua nafasi kujionesha kwamba wako sahihi. Unakuta wanatumia maneno kama vile “unajua sisi wanaume sio waongeaji kama wanawake”. Kwa hiyo kushindwa kwao kujieleza wanataka kukufanya kama kanuni ya maisha,. Yaani wanataka kila mtu ajue kwamba udhaifu wao uko sahihi.
Sasa hii haipo tu kwa wavulana bali hata linapokuja suala la pesa watu wanatafuta njia ya kuhakikisha kwamba wanajifariji ili wao waonekane kwamba wapo sahihi.
Kuna misemo ambayo maskini huitumia kujnionesha kwamba wapo sahihi. Mimi nasema kwamba wanajifariji, japo ukweli ni kinyume chake.
 Image result for rich and poor
HATA UWE TAJIRI KIASI GANI HUWEZI KUTEMBEA NA GARI KWENDA KITANDANI
Hii ni moja ya kauli ambazo watu huzitumia kila siku. Lengo lao ni kutaka kujionesha kwamba wapo sahihi kwa kutokuwa na pesa. Maana wanajifariji kwa kusema kama tajiri anatembea kwa miguu kwenda kulala basi hapo hakuna haja ya kuwa na pesa. Ila ukweli ni kwamba  kuna utofauti mkubwa sana.
Hata kitanda tu cha kulalia kati ya tajiri na maskini na tajiri kitakuwa tofauti, japo tajiri naye hutembea kwa mguu kwenda kulala. Lakini pia jambo bora sana ni pale unapoenda kulala bila hata ya kufikiria, kwamba pesa ya kula kesho utaitoa wapi. Hapa ndipo ilipolala tofauti kati ya matajiri na maskini.
HATA UWE NA PESA KIASI GANI HUWAEZI KUOGA NA NGUO ZAKO.
Huu nao ni msemo ambao wanautumia maskini kujipa moyo. Ila ukweli ni kwamba  hata kama wote hawaogi wakiwa wamevaa nguo, ila bado kuna utofauti mkubwa sana kati ya nguo anazovaa tajiri na zile anazovaa maskini, sehemu anapoogea tajri na sehemu anapoogea maskini.

Habari njema ni kwamba kuwa tajiri ni umamuzi ambao unaweza kuufanya leo hii. Ni umauzii  ambao haupapaswi kusubiri mtu ili uufanye sasa hivi. Amua sasa kuufanya mwisho wa siku utakuja kuwa kwenye hali nzuri sana ya kimafanaikio.

Wewe Ni Zaidi ya ulivyo sasa.
Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio.
Tukutane kwenye mzunguko wa wanamafanikio

Kujiunga na kundi la wasp la HAZINA YETU BONYEZA HAPA

Ndimi
Coach Godius Rweyongeza
godiusrweyongeza1@gmail.com
www.songambeleblog.blogspot.com


Ili kupata kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI  BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X