Huu Ndio Uhuni Hatari Unaofanyika Duniani


Habari ya siku hii ya leo rafiki na ndugu msomaji wa makala ya SONGA MBELE BLOG. Imani yangu kwamba leo ni siku njema sana kwako ambapo unaenda kuweka juhudi ili kuhakikisha unaongeza ufanisi katika kazi zako.
Katika dunia hii kuna uhuni mkubwa sana ambao huwa unafanyika kila siku. Uhuni huu umekuwa ukifanywa na watu bila kujua. Kwa kuwa uhuni huu unafanyika kila siku basi watu wameshauona kama sehemu ya pili ya maisha yao na pengine wanaukumbatia sana kama jambo la sifa sana. Sijui nani alianzisisha uhuni huu katika dunia hii ila ukweli ni kwamba uhuni huu unaharibu kizazi hiki.
Uhuni mwenyewe sio kwamba unafanywa na watu wengi sana. Ila ukweli ni kwamba uhuni huu unafaywa na mtu mmoja ambaye ni wewe. Ndio uhuni huuu unafanywa na mtu mmoja ambaye ni wewe. Bila shaka mpaka hapo utakuwa unajiuliza mimi huwa nafanya uhini gani? Uhuni ambao wewe hapo unaufanya  kila siku ni uhuni wa kupoteza muda wako.
Kila siku umejaliwa masaa 24 ambayo umepewa bure kabisa. Ila unachofanya ni kwamba unapoteza muda wako kila siku kwa kufanya mambo ambayo hayakujengi. Muda wako unaupoteza kufanya vile ambavyo havimo kwenye ratiba yako. Unapoteza muda mwingi ukiwaogelea watu wengine na pengine muda wako unawapa watu wengine. Hii yote ni habari mbaya sana ambayo inakuhusu wewe hapo ila unaweza kuirekebisha.
Unaweza kurekebisha na kuanza kuwa na matumizi mazuri ya muda kila kunapokucha kuanzia siku hii ya leo. Na haya hapa ni mambo ya muhimu ambayo unaaweza kuyafanya kuhakikishak kwamba unatumia vizuri sana muda wako kila siku.
#1. KUHAKIKISHA KWAMBA UNAPANGILIA SIKU KILA UNAPOAMKA ASUBUHI MPAKA UNAPOENDA KULALA.
Kila siku inayokuja mbele yako lazima itakuwa na kazi nyingi sana za kufanya hivyo hakikisha kwamba unapangilia kazi kila unapoamka asubuhi mpaka unapoenda kulala usiku. Anza kupangilia kazi zako kwa kuangalia kazi zenye umuhimu mkubwa sana kwako. Hili jambo jema sana ambalo unaweza kulifanya hasa pale unapoamka asubuhi.
#2. KUHAKIKISHA KWAMBA RATIBA AMBAZO HAZINA UMUHIMU MKUBWA SANA HAZIINGILII SIKU YAKO.
Wakati unaendelea na ratiba yako ya siku husika wanajitokekza watu ambao wanakuwa na ratiba tofauti tofauti. Hakikisha kwamba watu hawa hawaingiliii ratiba yako ya siku husika. Kama kuna mtu jambo la muhimu sana ambalo linahitaji wewe kulisikiliza basi unaweza kufanya hivyo. Ila kama hakuna ulazima basi unaweza kuacha.
#3. KUPANGA MUDA MAALUMU WA KUJIBU MESEJI ZA WATU KILA SIKU.
Kwa siku kuna watu wengi sana wanakutumia jumbe. Basi kwa sababu hiyo kila unapoamka mpaka unapoenda kulala unakuwa na jumbe nyingi sana ambazo unapaswa kujibu. Lakini habari njema ni kwamba ukiwa na muda maalumu wa kujibu jumbe fupi kama hizi hapa utaishi siku nzuri sana.  Wakati wa kujibu jumbe zako hakikisha kwamba unajibu jumbe ambazo unaona zina umuhimu mkubwa sana kwako.
#4. KUTEMBEA NA SAA.
Tembea na saa ambayo itakuwa inakuwambia kwamba muda wa kufanya jambo Fulani sasa umeisha unapaswa kuhamia katikajambo jingine. Hivyo hakikisha kwamba kila mahali ulipo una kuwa na saa yako ya mkoni ambayo itakukumbusha suala zima la muda.
#5. KUFANYA JAMBO MOJA KWA WAKATI.
Kama ambavyo hapo awali tumeona ni kwamba kwa siku unakuwa na vitu vingi sana vya kufanya. Lakini pia tukaona kwamba tunapaswa kuhakikisha kwamba tunapangilia kazi zetu kila siku asubuhi. Hapa tunaongeezea pointi nyingine kwamba  tunapaswa kufanya jambo moja kwa wakati. Ukigawa nguvu yako katika kufanya kazi jua kwamba kuna kazi ambazo hazitafanyika vizuri. Na kama baadhi ya kazi hazitafanyika vizuri basi jua kwamba matokeo pia hayatakuwa mazuri. Hivyo hakikisha kwamba unafanya jambo moja kwa wakati na kulikamilishaa
#6. KUACHA JAMBO LA KWANZA KUFANYIKA KWANZA.
“Kama kuna chura ambaye unapaswa kumla anza kumla chura mbichi” aliandika Brian Trancy katika kitabu chake  cha MLE CHURA HUYO. Chura mbichi ni kazi ngumu. Kila siku kuna kazi ambayo wewe unaona kama inakutisha. Kila asubuhi anza kwa kuifanya kazi hiyo. Hakikisha kwamba hautulii mpaka pale utakapokuwa umemaliza. Kama hiyo ni kazi  ya kwanza basi hata kazi ya pili hakikisha kwamba inafafuata kazi ambayo ugumu wake ni kawaida mpaka mwisho wa siku. Hivyo ndivyo ambavyo unaweza kupangilia ratiba yako ya siku husika ikakusaidia kufanya mambo makubwa sana ndani ya siku husika. Naomba sana nikutakie siku njema rafiki yangu.

Tukutane kesho kwa makala mengine kama ambayo yanaelimisha na kuhamasisha.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X