Je, kuna haja ya kuogopa hatari?


Miongoni mwa vitu ambavyo watu huwa hawapendi ni tendo la kufanya kosa. Watu wengi sana huwa hawapendi kufanya makosa wala kusikia kwamba wao wameshiriki katika kufanya makosa hayo. Ndio maana asilimia kubwa sana ya watu wengi sana huwa hawaweki malengo katika maisha yao kwa sababu tu  kwamba wanaogopa pale ambapo hawatatayatimiza itakuwaje. Lakini pia inakuwa sababu ya kwao kwamba hata kama watakuwa hawajatimiza malengo yao basi watakuwa na sababu ya kwa nini hawakutimiza malengo yao. Yaani watawambia watu kwamba hawakuwahi kuaandika malengo yao, na kwa sababu tu hawakuwahi kuandika malen go yao ndio maana hawakuyatimiza. Wenginea wawakuwa wanasema kwamba halikuwa jambo amabalo walikuwa wakilifikria katika maisha yao. Hivyo halina umuhimu. Hivyo wanajipa sababu ambazo hazina maana kuonekana kwamba ako wako sahihi kwa kutokuwa na malengo na wako sahihi kwa kutotimiza malengo yao.
Ila ukweli ni kwamba watu amabao hawana malen go wanapita katika maisha wakaitambaa kama viwavi. Yaani ndio kusema kwamba kuogopa  kuchukua hatua kutakufanya uendelee kuwa hapo hapo kila siku miaka nenda miaka rudi. Mbali na sababu kadha wa kadha ambazo tayari nimezitaja hapo juu ambazo zinawafanya watu wasiweke malengo yao katika maisha, leo hii naenda kuzungumzia sababu moja kwa undani ambayo inawafanya watu wasiweke malengo yao katika maisha yao. Sababu hiyo ni kwamba watu hao wanaogopa hatari.
Kuogopa hatari ni jambo ambalo linawafanya watu waendeleae kuwa hivyo hiyo kama ambavyo walivyo kila siku januari mpaka disemba.
Lakini swali la muhimu amb alo unapaswa kujiuliza ni je hatari zinaepukika maishani.
Jibu languu mimi GODIUS RWEYONGEZA ni kwamba hatari haziepukiki. Kila hatua ambayo mwanadamu anapiga inakuwa na hatari ndani yake. mtoto anapojifunza kutembea ni hatari kubwa sana. Lakini hata siku moja huwezi kusikia mzazi akimwambia motto wake kwamba unajua mwanangu sasa acha kutembea kwa sababu tu umeanguka. Bali mzazi anamtia moyo mtoto wa kuendelea kutembea mpaka pale atapokuwa amaeweza kutembea vizuri sana. Hii ndio kusema kwamba kama mtoto ataogopa hatari atapita katika maisha akitambaa kama kiwavi.  Ebu sasa achana na mtoto, njoo tu katika hali ya kawaida ya maisha na angalia matukio ambayo yanatokea kila siku katika maisha yako.
Gari linapoanza kutembea ni hatari, ndege inapopaa ni hatari, meli inaponoa nanga ni hatari, lakini pia wewe kutembea ni hatari. Kumbe hakuna kitu ambacho hakina hatari katika maisha. Kila sehemu kuna hatari kila mazingira yana hatari.
Tatizo la watu wengi linapokuja suala la hatari wapo ambao wanaongeza hatari na kuzifanya kuwa kubwa zaidi. Yaani hii ndio kusema kwamba hatari moja wanaikuza mara kumi zaid. Ndio usishangae kwa sababu huu ndio ukweli. Ngoja tu hapa nikupe mfano rahisi sana,
Kuendesha gari ni hatari. Ila kuendesha gari bila kushika usukani ni hatari zaidi. Sasa wanachofanya watu wengi katika maisha ni kuendesha gari bila kushika usukani. Hahahh! Unaona sasa, kumbe hatari hapa duniani haipo! Ila wewe kuachia usukani ndio kunafanya hatari iwe kubwa zaidi.
Sasa hapa ngoja niukuoneshe ni kwa jinsi gani unaweza kuzifanya hatari kuwa rahisi sana katika maisha yako.
#1. SAFIRI SAFARI AMBAYO UNAIPENDA
Katika maisha yangu sijawahi kukutana na mtu ambaye anakata tikaeti ya kwenda mwanza akiwa hataki kwenda mwanza. Hii ndio kusema kwamba asilimia kubwa sana ya watu wanaosafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine ni watu ambao wanasafiri kwa hiari  yao na kwa kupenda. Kumbe hii pia ni habari njema sana kwetu ambayo tunayo siku hii ya leo. Na wewe ukisafiri safari ambayo na wewe unaipen da, utaishi maisha mazuri sana. Ukienda sehemu ambayo unapenda utafika bila kuchoka. Kuna mtu mmoja aliwahi kusema kwamba ukifanya kazi ambayo unaipenda hutakuja kufanya kazi hata siku moja.
#2. JUA MWISHO WA SAFARI
Kila mtu ambaye anapanda basi lazima anajua kwamba safari yake itaishia wapi. Yaani kama yuko mbeya, ana kuwa na uhakika kwamba safari yake itaishia mwanza, kigoma au arusha. Je, wewe unajua mwisho wa safari yako ambayo unapaswa kuisafiri hapa duniani. Ukweli ni kwamba asilimia kubwa sana ya watu katika dunia hii hawajui safari  ambayo wanaisafiri inafananaje, lakini pia hawajui mwisho wa safari yao utakuwaje. Na ukitaka kujua hilo leo hii kafanye utafiti kwa kuwauliza watu swali hili hapa, “kitu gani na unapenda kutokana na makosa yake? Hapo sasa,  kwa kuuliza watu swali hil hapa utapata majibua ambayo yatakushangaza sana maishani mwako. Wapo watakaokumbia kwamba maishani mwao hawapendi makosa. Wapo watakakuambia kwamba wao sio watu wa kufanya makosa. Wapo watakaokuambia kwamba wao hawajawahi kufanya makosa na hawategemei kufanya makoa tena maishani mwao.
Kawaulize watu swali hili hapa. Lakini pia hakikisha kwamba unakuwa na ,mwisho katika maisha yako.
#3. JIFUNZE KUTOKANA NA MAKOSA.
Leo hii ukienda kkukata tiketi na ukakutana na tapeli ambaye atakukatia tiketi feki. Kesho yake ukaja kkupanda gari ukawa hulioni gari wala humwoni mtu ambaye amekukatia tiketi, kwako hilo linakuwa ni somo kubwa sana maishanai mwako. Hii ndio kusema kwamba hutakuja kurudia tena kosa kama hilo hapo. Badala yake siku nyingine kabla kabla hujakata tiketi, utahakikisha kwamba umewauliza watu kwa umakini wa hali ya juu sana. Mawali yako yote yatakuwa yaw ewe kutaka kujua ni kampuni gania ambayo unapaswa kukata tiketi. Lakini pia utaenda mbalai kwa kutaka kujua kwamba ili uje kwamba Yule aliyekukatia tiketi sio tapeli anapaswa kuwa na vigezo gani? Lakini pia ukishafika kwenye eneo la kukata tiketi utataka kuhakiki kwamba tiketi ambayo imekatwa inakuhakikishia wewe kusafiri siku ambayo utapenda kufanya hivyo.
Jambo hili linahitajika kkufanyika pia katika hali ya kawaida ya maisha. Yaani hii ndio kusema kwamba kama utafanya kosa leo hii. Hakikisha wkamba unajifunza kutokana na kosa hilo. Jambo hili hapa litakufanya wewe uzidi kusonga mbele.
Kwa le ohayo ndio ambayo ningependa kukushirikisha rafiki yangu. Imani yangu kwamba makala haya yatakuwa  yenye maufaa makubwa sana.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X