JE, MWANAMAHESABU WAKO NI NANI?


Tukiwa watoto wadogo, huwa tunaangalia wazazi wetu wanafanya nini! Huwa tunapenda kuangalia maisha ya watu wakubwa na kutaka kuiga. Hii inaweza kuwa kwa kufahamu au kwa kutofahamu. Lakini kujifunza kutoka kwa wazazi au wakubwa wetu ni jambo ambalo mtoto hawezi kulikwepa. Sasa kadri anavyoendeleaa kukua hali hii ya kuiga kila siku huwa inaendelea.

Ndio maana vijana wanaoangalia kwenye runinga na kutumia mitandao ya kijamii kuiga maisha ya watu wengine wanapata shida sana. Hii ni kutokana na ukweli kwamba wanataka kunakiri na kutumia kila kitu wanachokiona kutoka kwa watu wanaowaona mtandaoni. Yaani wanataka kunakiri kila kitu.

Kunakiri kila kitu sio kitu kibaya ila ubaya wake unakuja pale ambapo unakuwa hata hukai na kuanza kuchuja na kuja na kitu chako cha ziada. Unaruhusiwa kuiga ila sio kunakiri kila kitu kama kilivyo.

Ndio maana hata mtoto anayemwona baba yake kama baba bora akataka kuwa kama yeye. Atafanya vile vitu ambavyo baba yake alikuwa anafanya lakini bado kuna kitu kitamtofautisha yeye na baba yake.

Ukitaka kuwa kama mchezaji fulani, Fanya kama yeye lakini mwisho wa siku jitofautishe wewe kama wewe.

Kama mama yako alikuwa mwimbaji na wewe ukapenda kuwa mwimbaji, hata ufanyeje kuna kitu kitakutofautisha wewe.

Kumbe ukishakifahamu hiki kitafute na hakikisha unakifanyia kazi.

Katika  maisha yako hakikisha unakuwa na watu ambao wanaitwa ROLE MODELS kwa lugha ya wenzentu. Ila usichukue kila kitu katoka kwao. Unaweza kuwa hata na picha zao kwenye daftari lako la dhahabu (daftari lako la malengo).

Kwani hawa watu wana msaada gani?
Hawa watu wana msaada mkubwa sana.

Hapa nipo nataka nikukumbushe enzi zileee za shule ya msingi na sekondari!!!

Kama mwanafunzi angeambiwa anamfanana mwalimu fulani na mwalimu yuke akawa anajua kiingereza basi mwanafunzi huyo alikuwa anajitahidi kuongea kiingereza hata kama hajui ili awe kama mwalimu waliyesema anajua kiingereza vizuri.

Au pengine ungesikia mwanafunzi anaambiwa umezaliwa siku moja na mwanamahesabu fulani (Phythogras). Basi mwanafunzi huyo alikuwa anajitahidi kufanya hesabu hata kama zingekuwa ni ngumu sana. Hapa alitaka kuonesha kwamba asije akamwangusha yule mwanamahesabu mwenzake aliyezaliwa naye siku moja.

Au kama mwingine alikuwa na jina la mtu fulani maarufu. Mfano NEWTON basi yeye na fizikia ulikuwa humwambii kitu. Alikuwa anataka kuonesha kwamba akina NEWTON ni wanafizikia.

Mwingine angeambiwa wewe umezaliwa mwezi fulani na mtu fulani maarufu basi anaanza kusema mwezi fulani ni mwezi wa magenius.

Sasa ndio maana nakwambia na wewe tafuta role model wako. Unaweza kuwa na hawa ma role model katika sekta tofauti tofauti.

Jifunze kutoka kwao ila usichukue kila kitu kutoka kwao.

Kama wewe unataka kuwa mwanamziki, mwanamziki wako maarufu ni nani?

Wewe mwanafunzi unataka kuwa mwanamahesabu, mwanamahesabu wako ni nani?

Sina shaka wewe ukiambiwa ni kama kiongozi fulani maarufu mfano Nyerere, Obama au Mandela utajiyahidi kufabya kama yeye amua, sasa, chukua hatua leo, wewe zaidi ya ulivyo leo.

Wewe Ni Zaidi ya ulivyo sasa.
Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio
Kujiunga na kundi la wasp la HAZINA YETU BONYEZA HAPA
Ndimi
Coach Godius Rweyongeza
godiusrweyongeza1@gmail.com
www.songambeleblog.blogspot.com
Ili kupata kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI  BONYEZA HAPA

Bonyeza hapa ili uweze kupata makala maalumu kila wiki.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X