Kanuni Tatu Ambazo Unahitaji Kuzifahamu Ili Uweze Kufanya Makubwa Mishani Mwako


Habari ya siku hii ya leo rafiki na ndugu msomaji wa makala ya SONGA MBELE. Imani yangu kwamba leo hii ni siku njema sana kwako ambapo unaenda kuweka juhudi kubwa sana kuhakikishakwamba unaweza kufikia mafanikio makubwa sana. Kanuni za mafanikio sio kwamba zimebadilika. Bado ziko vile vile kama ambavyo zimekuwa kwa miaka mingi sana ambayo imepita. Hivyo ni jukumu letu kuhakikishakwamba tunazifuata kanuni hizi ili tuweze kufikia mafanikio makubwa sana maishani mwetu.
Siku zote huwa napenda kuwaambia watu kwamba ukizijua kanuni za kitu fulani hautakuja kuhangaika maisha yako yote, yaani utaishi maisha mazuri sana yenye furaha na yanayopendeza. Kumbe, siku zote tafuta kuzijua kanuni, tafuta kujua ni kwa jinsi gani unaweza kuzitumia kanuni kwa manufaa yako sio jinsi gani unaweza kuzivunja kanuni. Kama wewe ni mkulima, jifunze kanuni za kilimo. Kama wewe ni mchezaji wa mpira wa miguu jifunze kanuni za mchezo wa mpira wa miguu. Na kama unacheza mchezo wa biashara kanuni zake zi wazi, hivyo hakikisha kwamba unajifunza kanuni hizi hapa ili ziweze kukunufaisha. Katika makala haya nitakushirikisha kanuni kubwa tatu ambazo kwa leo unapaswa kuhakikisha kwamba unazifahamu. Ubora wa kanuni hizi ambazo nitazifundiha siku hii ya leo zinafanya kazi katika kila sekta ya maisha, yaani zinafanya kazi katika kila nyaja ya maisha.
Zitumie vizuri kanuni hizi kwa ajili ya manufaaa yako.
#1 OTA NDOTO KUBWA ILA ANZA NA KIDOGO
Kuwa na mafanikio makubwa sana maishani mwako ni mchakato ambao unahitaji kuhakikisha kwamba umeufahamu. Mchakato huu unaanzia kwako siku zote na unaishia kwako. Unaanzia kwako kwa mantiki ya kwamba wewe ndiwe mtu ambaye unahitaji kuhakikisha kamba una ndoto kubwa sana. Kuwa na ndoto kubwa hakukuzuii wewe kuanza. Unapaswa kuwa na ndoto kubwa sana. Ila uanzaji wake unakuwa wa tofauti na watu wengine wanavyotegemea. Wakati wengine ukiwaaambia kwamba mimi hapa ninayo ndoto kubwa sana wanaona kwamba haiwezekani. Wewe hapo unapaswa kuhakikisha kwamba unaanza na kidogo juu yakile ambacho unakifanya. Endelea na hicho kidogo na hakikisha kwamba unakikuza ili kiweze kuwa chenye manufaa makubwa na mafanikio makubwa hapo mbeleni.
Ndoto yoyote kubwa huwa haianzi kwa ukubwa wake. Isipokuwa huwa inaanza kwa udogo wake ambao unalenga kuboreshwa na kukuzwa ili iweze kuwa ndoto kubwa sana.
#2 TATUA TATIZO KUBWA SANA
               Kama katika jamii yako kuna tatizo kubwa sana ambalo wewe hapo unaweza kulitatua, na kwa ubora wa hali ya juu sana. Usiliache. Endelea nalo na hakikisha kwamba unalitatua tatizo hili kadri uwezavyo. Watu wanapenda matataizo yao  yatatuliwe kwa njia ambazo ni rahisi sana. Watu hawapendi kusumbuka na kuahanganika muda mwingi wakitafuta huduma. Hivyo kanuni yetu ya pili kwa siku hii ya leo ni kwamba hakikisha unatatua tatizo kubwa sana ambalo linawakabili watu.
Mwanzilishi wa google aliona kwaba kuna tatizo kubwa sana ambalo linawakabili watu. Tatizo lenyewe ni ukosefu wa taarifa na upatikanaji wake. Hivyo aliamua kuhakikisha kwamba  anawaletea watu huduma kubwa ambayo ingeweza kuwasaidia watu kutatua matatizo yao ambayo walikuwa nayo. Kwa kufanya hivyo akawa ametatua matatizo makubwa sana ya watu kwa kutoa huduma kkubwa illiyokuwa inatataua matatizo ya watu. Je, wewew jamii yako ina matatizo gani ambaytayo unaweza kuanz nayo kuyatkatua illi jamii yako iwezse kukullipa?
#3 THAMANI YA HUDUMA YAKO
Hakikisha kwamba unatoa huduma yenye thamani kubwa sana. Huduma yenye thamani kubwa sana itawavuta watu zaidi kuja kwako. Na kwa kufanya hivyo itaweza kukuondolea washindani ambao wangeweza kujitokeza.
Kwa hiyo wakati unatoa huduma jiulize swali hili hapa la muhimu sana. Je, tatizo ambalo watu wanalo linaendanana na huduma ambayo mimi hapa ninatoa? Kama jibu lako ni hapana hakikisha kwamba unaendelea kutoa huduma zaidi na zaidi.

Hizo ndizo kanuni tatu ambazo unahitaji kuhakikisha kwamba umezifahamu kwa siku hii ya leo. Endelea kujifunza kanunai zaidi na zaidi kila kunapokucha. 
Wewe Ni Zaidi ya ulivyo sasa.
Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio.
Tukutane kwenye mzunguko wa wanamafanikio
Kujiunga na kundi la wasp la HAZINA YETU BONYEZA HAPA
Ndimi
Coach Godius Rweyongeza
godiusrweyongeza1@gmail.com
www.songambeleblog.blogspot.com
Ili kupata kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI  BONYEZA HAPA

Bonyeza hapa ili uweze kupata makala maalumu kila wiki


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X