Ni mara nyingi sana tumesikia juu ya sheria ya asili ya kichocheo na matokeo. Ni mara nyingi sana umeambiwa ukitaka kupata kile unachokitaka lazima utengeneze mazingira. Lakini mpaka sasa kila mtu amekuwa akilalamika huku akitoa hadithi zile zile za haya siyawezi bwana. Hivi viti sio vya viwango vyangu. Na mambo mengine kama hayo. Kwa sababu hiyo leo hii nimeamua kuzungumzia jambo moja linalowarudisha watu kila siku nyuma.
Jambo ambalo kila mtu akilifahamu basi atakuwa na maendeleo makubwa na ataweza kujiinua na kuwa zaidi ya alivyo sasa.
Jambo lenyewe ni KUTHUBUTU.
Soma zaidi; Sababu Mbili Zinazowafanya Watanzania Wazidi Kurudi Nyuma Linapokuja Suala La Mafanikio
Kuna watu wanaogopa kuthubutu na kuchukua hatua za kuwatoa sifuri kuwapeleka kileleni. Wanadhani kuna mtu akiwaona basi atawahurumia na kusema njoo hapa maana unafaa sana.
Ninachojua mimi hapa duniani hakuna amayekuonea huruma wewe. Wewe mwenyewe ndiwe unapaswa kujionea huruma. Hakuna atakayejua kwamba una ujuzi fulani mpaka pale utakapochukua hatua madhubuti kuhakikisha unauonesha ujuzi wako.
Kwa hiyo kama wewe unasema una ujuzi hakikisha unatoka hapo ulipo na kwenda mbele zaidi ili uoneshe huo ujuzi wako. Tembea kwa kujiamini na kila utakayekutana nawe hakikisha hapiti katika mikono yako bila ya wewe kumwambia kwamba mimi Nina ujuzi fulani. Nenda mbele zaidi. Thubutu kwa kila kitu maana wewe unaweza. Watu waliofikia mafanikoo makubwa ni wale wanaothubutu. Laiti kama utaendelea kutamani mafanikio bila kuchukua hatua kwa kuthubutu. Basi utaendelea kusikia mafanikio kwenye vyombo vya habari.
Kuna watu walistahili wawe wamepiga hatua kubwa sana kimaisha. Lakini kutokana na ukweli kwamba hawathubutu ndio maana wako hapo walipo. Wewe hutakiwi mmoja wao.
Thubutu leo.
Chukua hatua leo.
Nenda hatua ya ziada leo.
Tukutane kileleni.
Soma Zaidi; Jifunze Kuwasiliana
Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio.
Tukutane kwenye mzunguko wa wanamafanikio
One response to “Kitu Kimoja (01) Kitakachokuinua Leo Na Hii”
Asante kaka Godius