KONA YA SONGA MBELE; Jinsi Ya Kuongeza Ufanisi Kazini -2


Habari ya siku hii ya leo rafiki na ndugu mfuatiliaji wa makala haya murua kutoka katika blogu yako pendwa ya SONGA MBELE.

Kama ilivyo ada siku ya jumapili huwa tunapata Makala maalum ambayo huwa yana kichwa cha kona ya SONGA MBELE.

Wiki iliyopita tulipata kuanza kuangalia mfululizo wa makala maalumu ambayo yanalenga kutufanya tuongeze ufanisi kazini.

Ikumbukwe katika zama tulizopo  haulipwi kwa kiwango  cha muda wa kufanya kazi, Lakini unalipwa kwa kiwango cha ufanisi wa kazi zako.

Lengo kubwa la Makala haya ni kukuongezea ufanisi kazini kwako, bila hata kutumia muda mwingi sana kazini kwako. Kumbuka kanuni hizi zinafanya kazi kwa watu wote uwe mwanafunzi, mwanachuo, mwajiriwa, mjasiliamali, mjasiliapesa, mwandishi, mfanyabiashara au mwekezaji kutaja ila wachache. Kanuni  pia zinafaya kazi uwe Afrika, Ulaya, Marekani, Urusi au Asia. Kwa hiyo hakikisha unazielewa kanuni hizi, ambazo zimetumiwa na watu walioweza kufikia ufanisi mkunwa sana kazini kwao.

Leo tunaangalia kanuni inayoitwa kanuni ya THEMANIMI ISHIRINI. 80/20

Kanuni hii inasema kwamba, asilimia kubwa sana ya kazi unazofanya ambazo ni asilimia (80%) inachangia kuleta matokeo makubwa sana ambayo ni sawa na asilimia (20%). Na kazi ndogo sana ambazo unazifanya ambazo ni sawa na asilimia (20%) zinachangia kuleta matokeo makubwa sana ambayo ni sawa na asilimia (80%).

Kumbe kati ya kazi nyingi sana ambazo unafanya ni asilimia kidogo sana ya kazi ambazo zinachangia matokeo makubwa sana.
Kuifahamu kanuni hii kunakufanya upunguze wingi wa kazi unazofanya na kushughulika na kazi kidogo sana. Kazi ambazo zitaongeza ufanisi.

Hii ndio kusema kwamba kati ya kazi kumi unazofanya kila siku. Mbili tu ndio kazi zenye umuhimu mkubwa sana kwako. Nyingine hazina umuhimu mkubwa sana.

Hivyo hakikisha kwamba kila unapoianza siku yako unajiuliza je, kazi zipi zinachangia mafanikio makubwa sana kwangu. Je, ni kazi gani ambazo hata kama sitazifanya siku hii ya leo hazitakuwa na madhara kwenye kazi yangu. Je, kazi zipi sipaswi kuzifanya mimi mwenyewe na badala yake zinaweza kufanywa na mtu mwingine. Chukua hatua na anza kuitumia kanuni ya inayokuhitaji kufanya kazi kidogo zenye mchango mkubwa sana katika kazi yako.

Kanuni hii ya themanini ishirini themanini au themanini ishirini inafanya kazi kila sehemu na katika kila sekta. Tukutane siku nyingine katika Makala mengine kama haya.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X