Habari ya siku hii ya leo Rafiki na ndugu msomaji wa makala haya ya SONGA MBELE. Imani yangu siku ya leo imekaa vizuri sana, na unaendelea kujifunza zaidi na zaidi kuhakikisha kwamba unaongeza ufanisi kazini kwako.
Makala za kila jumapili ambazo zinakuja katika kichwa cha kona songambele zimelenga jambo hilo. Leo hii tunaenda kuangalia SHERIA YA VICHACHE VYENYE MATOKEO MAKUBWA. Sheria hii ya vichache vyenye matokeo makubwa sana ni mwendelezo wa kanuni ya THEMANINI ISHIRINI (80/20). Kama hukubahatika kusoma makala haya basi unaweza kubonyeza hapa ili usome makala ya wiki iliyopita kwanza.
Katika makala ya wiki iliyopita tuliona ni kwa jinsi gani unapaswa kupunguza kazi kwa kufanya kazi kidogo sana zinazoongeza ufanisi mkubwa sana kazini kwako.
Baada ya kupunguza kazi na kuona kwamba kazi ndogo sana ndizo zinzongeza yfanisi. Kinachofuata ni kupunguza zaidi. Unahitaji kupunguza tena. Usishangae ndivyo ilivyo.
Kama ulikuwa unafanya kazi ishirini na ukagundua kwamba kazi nne tu ndizo zinazoongeza ufanisi mkubwa basi punguza tena. Kati ya hizo kazi nne, punguza hadi mbili ambazo utaona zinakufaa sana. Kwa hali hii utakuwa umefikia kiasi kikubwa sana cha kuitumia kanuni ya vichache vyenye matokeo makubwa sana.
kumbe hii ndio kusema kwamba miongoni mwa kazi nyingi sana unazofanya kila siku basi kazi moja tu ndio yenye uzito mkubwa sana ndio unahitaji kuipa muda wako mwingi katika kuifanya. hii ndio siri ambayo watu wengi sana wamekuwa hawaijui. siri inafahamika kwa watu wachache sana, na wanaoifahamu siri hii ndio wanaofikia mafanikio makubwa. hii ni kutokana na ukweli kwamba watu hawa wanakuwa na ufanisi mkubwa sana kazini. ila ubora ni kwamba kama hawa wamewewza basi nawewe unaweza kufanya makubwa zaidi.