Kwa Nini Wanafunzi Wanaopata “A” Wanawafanyia Kazi Wanafunzi Wanaopata ‘C’, Na kwa Nini Wanafunzi Wanaopata “B” Wanaifanyia Kazi Serikali
(Why A Student Work For C Students, And B students Work For Government).
Ulikuwa mwezi wa tano mwaka huu 2017. Nikiwa katika viwanja vya freedom square katika chuo kikuu cha SUA. Hapo nilikiwa namsikiliza Joel Arthur Nanauka katika semina iliyokuwa inaendelea kwenye viwanja hivyo. Joel Nanauka alikuwa akieleza Four insights for acquiring the right mindset that will help you aquire your goal. Nilimsikiliza kwa umakini sana.
Wakati anaendelea kuzidadafua hizo insights nne. Alitaja Kitabu kimoja ambacho nilikuwa sijawahi kukisoma. Kitabu ambacho kimeandikwa na mwandishi ambaye namfuatilia sana, Robert Kiyosaki.
Nilipenda sana title ya kitabu.
Baada ya semina nikiwa chumbani kwangu natafakari nilichojifunza kwenye semina, Mara simu ikaita. Kuangalia simu ni Edius Katamugora anapiga. (Edius katamugora ni mwandishi wa Kitabu cha Barabara ya Mafanikio). Nilipokea simu na maongezi yakaanza. Wakati wa maongezi yetu nilianza kumweleza Edius Katamugora juu ya somo la ambalo lilitolewa na Joel Nanauka. Ndipo nikamwambia kwamba nilisikia akizungumzia habari za Kitabu chenye kichwa cha Why A Student Work For C Students, And B students Work For Government. Edius aliniambia kwamba tayari kakisoma na ni Kitabu Kizuri sana. Alisihi nikisome na akaahidi kunitumia na mimi.
Je, nilikisoma? Kutokana na ratiba zangu kuwa vitu vingi ambavyo nilikuwa nimepangilia, lakini pia tayari nilikiwa nimepangilia vitabu ambavyo nilipaswa kuvisoma sikukisoma. Miezi mitatu baadae wakati naongea na Edius aliniuliza kama tayari nilikuwa nimesoma Kitabu hicho, ndipo nilimpa taarifa kwamba bado ila nitakifanyia kazi muda si mrefu.
Nilichukua hatua na sasa naenda kukushirikisha mambo niliyojifunza kwenye Kitabu hicho.
Soma Zaidi; Ndoto Kutoka Kwa Mama Yangu, Ndoto Kutoka Kwa Mwalimu Nyerere
Swali,
Kwa nini wanafunzi wanaopata A wanawafanyia kazi wanafunzi wanaopata C, na kwa nini Wanafunzi wanaopata B wanaifanyia kazi serikali?
Elimu inayotolewa shuleni sio elimu ambayo inwandaa mwanafunzi kujua matumizi sahihi ya pesa. Kuna watu wanakuwa magwiji katika uwanja wa shule lakini si wote. Hii haimaanishi kwamba wale ambao si magwiji katika uwanja wa shule hawawezi kuwa magwiji. La hasha! Kila mtu ana eneo ambalo anaweza kuwa gwiji na kufanya mambo makubwa. Mwandishi anawekea mkazo suala hili kwa kuutumia msemo wa Albert Einstein “kila mtu ni gwiji. Tatizo ukimhukumu samaki kwa uwezo wake wa kupanda mti, ataishi maisha yake yote akiamini kwamba yeye ni mjinga”
Mfumo wa elimu ni mfumo ambao unabadilika taratibu sana kuliko mifumo mingine yoyote. Inachukua miaka 50 wazo la maana kuanza kufanyiwa kazi. Wakati mifumo mingine kama ya teknolojia huchukua miezi 18 tu. Ndio maana kila wakati unapata vyombo vipya vya kielektroniki. Mfano simu za tekno zinabadilika Mara kwa mara, C5, C8, C9 n.k. hii ni kutokana na ukweli kwamba sekta hii inabadikika haraka kulinganisha na sekta nyinginezo kama ya elimu.
Hata hivyo sekta ya elimu ina magwiji wengi ambao wamekuzwa na mfumo huo na bado wanaamini ni mfumo sahihi ndio maana ni vigumu mfumo huu kubadilika.
Wanafunzi wanaopata C ndio wanafunzi ambao wanashinda katika maisha hii ni kutokana na kwamba;
Soma Zaidi; Sababu Mbili Zinazowafanya Watanzania Wazidi Kurudi Nyuma Linapokuja suala La Mafanikio
1. Wanasoma Kile ambacho wanafunzi wanaopata A hawasomi.
Siku zote nyumbani na shuleni utaambiwa nenda shuleni usome, ili upate kazi inayolipa sana kwenye kampuni zuri.
Ila Maarifa ya matumizi na jinsi kuitumia pesa hautayapata shuleni. Wanafunzi wanaopata C huyatafuta Maarifa haya ndio maana huwatofautisha wao.
2. Njia nzuri ya kumfundisha mtoto kuhusu pesa ni Kumfundisha kwa vitendo. Badala ya kukaa na kuanza kumwambia pesa infanya kazi hivi. Onyesha kwa vitendo ili na yeye aone. Vitu vinavyofundishwa kwa vitendo vinakumbukwa sana kuliko vinavyofundishwa kwa maneno tu.
4.. Watoto hupitia madirisha matatu ya ukuaji. Ndani ya madirisha haya watoto huwa wanajifunza mambo mbali mbali. Ni muhimu mzazi kuyafahamu madirisha hata na kuanza kuwamwandaa mtoto wako katika ulimwengu wa kipesa akiwa bado mdogo.
a) DIRISHA LA KWANZA (MIAKA 0-12).
5. Hiki ni kipindi ambacho ubongo wa mtoto unakua na ni kipindi ambapo mtoto huwa anajifunza vitu vingi vipya. Mfano mtoto hujifunza lugha, kutembea, kuendesha baiskeli n.k
6. Ni muhimu sana ndani ya kipindi hiki mzazi ukaanza kumfundisha mtoto wako mambo muhimu kuhusu pesa.
b) DIRISHA LA PILI (MIAKA 12-24)
7. Hiki ni kipindi ambacho mtoto hujifunza kwa kupinga sana. Ndani ya kipindi hiki ukimwambia mtoto, usilewe basi yeye atataka kulewa ili aone itakuwaje. Ukimwambia usivute sigara, au usijihusishe na mapenzi, yeye atapinga na kufanya kile ulichosema asifanye.
Sasa mwitikio wako wewe kama mzazi juu ya kile ambacho anafanya ndio unaweza kumfanya mtoto mwema au kumharibu zaidi.
7. Mtoto akija kwako na mimba mzazi utasemaje ndani ya kipindi hiki?
Mtoto akiletwa kwako kaiba utachukua hatua gani ndani ya kipindi hiki?
Mtoto akikamatwa na polisi kwamba anauza madawa ya kulevya, mazazi nini hatua utachukua?
Hapa hakuna majibu ya moja kwa moja kwa kila mzazi. Ila ni muhimu mzazi kutokurupuka kumtetea mtoto haswa pale anapokutwa na makosa.
8. Badala ya kuwambia mtoto usifanye hiki. Muulize maoni yake juu ya mambo mbali mbali ya kimaisha.
Mfano badala ya kumwambia “usilewe”, “usivute bangi”, “usijihusishe na mapenzi”.
Mwambie unafikiri ni nini madhara ya «kulewa», «kuvuta bangi» na «kukihusishana mapenzi»
c) DIRISHA LA TATU (MIAKA 24-36)
9. Ndani ya kipindi hiki ndipo watoto hutafuta njia sahihi ya maisha. Kazi ya maisha ambayo inawafaa. Hivyo utakuta mtoto akijaribu kufanya kazi hii na kuacha. Jukumu lako kama mzazi ni kumpa mwongozo vitu sahihi ambavyo vitampeleka kule anapopataka.
10. Usimchagulie mtoto wako kazi gani afanye. Wala usimlazimishe kuingia kwenye Biashara. Mweleze kwa umakini ni sehemu gani ambapo akifanya kazi atapata kipato Kizuri na kulipa kodi vizuri, ila mwache yeye ajichagulie kama anataka kuwa mwajiriwa, kujiajiri, mfanyabiashara au mwekezaji.
11. Utafiti unaonesha kwamba 33% ya kati ya watu 400 ambao hutokea kwenye gazeti LA forbes hawakwenda chuo au hawakumaliza chuo.
Wanafunzi waliohitimu chuo na maksi nzuri hufanya vibaya katika maisha kwa sababu tu, shule waliambiwa hawapaswi kufanya makosa.
Ndio maana hata kama wanafunzi hao watafanya kazi kwa bidii, kujituma na kuweka juhudi ila mwisho Wa siku utakuta wanaogopa sana makosa.
12. Huwezi kumfundisha mtu na kumpa mtu mbinu za utajiri, mpaka yeye aamue mwenyewe. Ukimfundisha mtu kitu ambacho hapendi mlango wa kujifunza hujifunga, ukimfundisha mtu kitu anachopenda mlango Wa kujifunza hujifungua.
13. Kama unataka kubadili maisha, badili mtazamo.
Kama unataka kuwa tajiri anza kufikiro jinsi ambavyo matajiri wanafikiri. Maskini hufikiri kama masikini na watu Wa kipato cha kati hufikiri kama watu Wa kipato hufikiri kama watu Wa kipato cha kati! Je, wewe unataka kufikiri kama nani?
Haya ni mambo machache sana kati ya mengi ambayo nimejifunza katika kitabu cha kwa nini wanafunzi wanaopata A wanawafanyia kazi wanafunzi wanaopata C na kwa nini wanafunzi wanaopata B wanaifanyia kazi seriakali. Ni muhimu sana wewe kuhakikisha kwamba unachukua nakala ya kitabu hiki na kukisoma wewe mwenyewe. Utapata kujifunza mambo mengi sana ambayo wanafunzi wanaopata C wanayafanya huku yakiwa hayafanywi na wanafunzi wanaopta A
Nikutakie siku njema. Tukutane siku nyingine kwenye makala nyingine zaidi zinazoelimisha na kuhamasisha.
Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio.
Tukutane kwenye mzunguko wa wanamafanikio
6 responses to “Kwa Nini Wanafunzi Wanaopata “A” Wanawafanyia Kazi Wanafunzi Wanaopata ‘C’, Na kwa Nini Wanafunzi Wanaopata “B” Wanaifanyia Kazi Serikali”
Asante kocha umenena vyema kiongozi. Ubarikiwe sana kwa kuendelea kuilisha akili yangu madini adimu.
The lesson seem to be interesting but it lacks your position as a reviewer.
What do you undestand by the 33% of 400 people in LA forbes and what do you understand by success? Is it always successful individual is measured in monetory terms?
I like the way you have shared it but I think we need to try showing our positions quite clear if in fact we are teaching.
And go and read about theorem and the impact of social context to the lives of individual. I hope you will be able to make stronger judgements which will help us young and parents. Thank you
*Theory instead of theorem
This comment has been removed by the author.
[…] SOMA ZAIDI: Kwa Nini Wanafunzi Wanaopata “A” Wanawafanyia Kazi Wanafunzi Wanaopata ‘C’, Na kwa Nini Wana… […]
[…] Kwa Nini Wanafunzi Wanaopata “A” Wanawafanyia Kazi Wanafunzi Wanaopata ‘C’, Na kwa Nini Wana… […]