Maswali Muhimu Ya Kujiuliza Kabla Kuingia Katika Uasiliamali


Ujasiliamali sio tu suala la lelemama kwamba unalala usiku na kuamka asubuhi ukisema mimi ni mjasiliamali. Ujasiliamali unapitia hatua. Ukiingia katika ujasiliamali kichwa kichwa unaweza kukata tamaa sana na pengine kuamua kuacha kabisa suala  huku ukisema kwamba mimi siwezi kuwa mjasiliamali.
Kuna watu wengi wameingia katika ujasiliamali wakitegemea kwamba uujasiliamali uwe wenye manufaa makubwa sana maishani mwao. Ila walichosahau ni kwamba si ujasiliamalia ambao unapaswa kukufaaa ila wewe unahitaji kuufaa ujasiliamali. Kwa hiyo kama wewe unaona huufai ujasiliamali afadhali uache kabisa. Maana unaweza kuingia katika ujasiliamali ukijua unaenda kucheza mechi katika uwanja wa nyumbani kumbe wewe unaaenda kucheza mechi katika uwanja wa ugenini. Ndio maana sio kila mtu ni mjasiliamali.
Watu wengine wameona ujasiliamali hauwafai na wakaamua moja kwa moja kubeba majukumu ambayo wao wanaona yanawafaa. Ndio kuna watu wengine ni walimu, wengine ni madaktari, wengine ni wahandishi na wengine ni waaandishi. Hawa ni watu ambao wameona kwamba ujasiliamali sio uwanja wa nyumbani. Wameamua kuutafuta uwanja wao wa nyumbani ili waweze kucheza mpira vizuri. Kwa hiyo kiufupi ni kwamba ukimwona dakatari jua kwamba uwanja wake wa nyumbani ni kwenye utabibu. Ukimwona mhasibu jua kwamba uwanja wake wa nyumbani ni kwenye utunzaji wa pesa. Ukimwona mjasiliamali jua kwamba uwanja wake wa nyumbanii ni kwenye kuanzisha na kukuza biashara ndogo ndogo. Je, wewe uwanjwa wako wa nyumbani ni upi?
Haya hapa ni maswali muhimu sana ambayo unahitaji kujiuliza kabla ya kuingia katika ujasiliamali? Kama utweza kuyajibu maswali haya kwa uhakika basi jua kwamba utakuwa katika njia ya kuwa mjasiliamali makini sana.
1.      Je, upo tayari kufikiri mwenyewe na kuja na mawazo mapya ambayo ni ya toofauti kabisa? Hapa unahitaji kufahamu kwamba biashara zinabadilika kila siku. Lakini pia mbali na kwamba biashara zinabadilika bado unahitaji kuhakikisha kwamba unajitofautisha mwenyewe. Kama utafanya biashara kwa namna ya kiamazoea ambayo kila mtu anafanaya basi hapo jua kwamba utakuwa umejipoteza. Unahitaji kuhakikisha kwamba ujaitoautisha. Na njia nzuri ya kujitifautisha wewe mwenyewe basi ni kukaa chini na kufikiri.
Kama jibu lako ni ndio basi hapo jua kwamba  na maksi 90%
Kama utasema kwamba namtegemea mtu aniazalishie mawazo basi hapo una asilimia 40%
Na kama katika jibu lako utassema kwamba namsubiri mtu wa kunizalishia mawazo. Basi hapo utakuwa na asilimia 10%
2.      Je, upo tayari kuchukua hatua za hatari? Kuna hatua ambazo utahitaji kuzichukua kila siku ambazo watu wengine wanaona kwamba ni za hatari ila wewe kama wewe unaona ni kawaida. Kuna hatua ambazo watu wanaogopa kuzichukua ambazo wewe mjasiliamali unahitaji kuhakikisha kwamba umeweza kuzihimili.
Kama utasema napenda kuwa katika meno ya msumeno hapo una asilimia 90%
Kama jibu ni itategemea  basi hapo jua kwamba una asilimia 40%
Na kama utasema huwa sipendi usumbufu basi jua hapo una asilimia 10%
3.      Swali la tatu na muhimu sana ambalo unahitaji kujiuliza kabla ya kuanzisha biashara, ni je,wewe ni kiongozi?
Ujasiliamali unahitaji mtu ambaye ana uwezo wa kuongoza watu wengine. Mtu ambaye ana ushawishi. Hii ni kutokana na ukweli kwamba mjasiliamali huwa anawaongoza watu ambao hawawezi kuchukua maamuzi kama ambavyo yeye anafanya. Mjasiliamali anahitaji kuwa na roho ya kiungozi kwa sababu anawaongoza watu ambao wameandaliwa katika nyanja tofauti tofauti. Yaani unakuta katika biashara kuna wasomi, ambao hawajaennda shule, watu ambao wanaongea sana na watu ambao ni wabunifu. Haya yote yanakuhitaji uwe kiongozi ili uweze kuwaunganisha watu mbali mbali wenye mitazamo tofauti tofauti ili kuwa kitu kimoja na kuja matokeo bora katika biashara yako.
Kama utajibu ndio basi utakuwa na asilimia 90%
Kama utajibu ndio lakini pale ambapo itakuwa lazima basi hapo utakuwa na asilimia 40%
Kama jibu lako ni hapana basi hapo utakuwa na asilimia 10%
4.      Je, unaweza kuishi bila kutegemea mshahara?
kuna wakati biashara yako haitaenda kama ambavyo ulikuwa unatarajia. Kuna wakati utahitaji kuhakikisha kwamba unawekeza nguvu na juhudi kubwa sana ili uweze kufanikisha kile ambacho unakifanya. Kuna wakati utahitaji kuweka pesa katika biashara yako ili uweze kuikuza huku biashara yakoo ikiwa haiingizi hata senti. hapo ndipo umuhimu wa swali la nne unatokea. Je, unaweza kuishi bila ya kuwa na mshahara?
Kama jibu lako ni ndio. Basi hapo utakuwa na asilimia 90%
Kama jibu lako ni pale itakapobidi basi hapo utakuwa na asilimia 40%
Na kama jibu lako ni hapna basi jua kwamba hapo utakuwa na asilimia 10%
5.      Je, unaweza kumfukuza mtu ambaye hajafanya vizuri kazi ambayo umempatia?
Sio kila kazi utafanya wewe. Kuna watu utawahitaji kuhakikisha kwamba wanakusaidia wewe hapo kufanya kazi. Hawa watu wanaitwa waajiriwa. Je, upo tayari kuwafukukza kazi pale amapo hawatafanya kazi vizuri?
Kama jibu ni ndio basi jua kwamba hapo una asilimia 90%
Kama jibu lako ni mimi naogopa kufanya maamuzi kama hayo jua kwamba una asilimia 40%
Kama jibu lako ni siwezi kabisa. Basi jua kwamba hapo utakuwa na asilimia 10%
Hayo hapo ni maswali muhimu ambayo unahitaji kujiuliza vizuri wewe kama mjasiliamali na kuhakikisha kwamba umeweza kuyajibu vizuri. Jiulize mara nyingi sana maswali haya. Jiulize kila siku maswali haya. Mpaka pale utakapokuwa umepata majibu sahihi. Hapo ndipo utapaswa kufanya maamuzi ya wewe kuingia katika ujasiliamali. Muda ndio huu hapa. Chukua hatua sasa ili uweze kufanya kitu ambacho ni bora siku hii ya leo.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X