TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA-63


Tatizo hujajua umuhimu wa jina lako

Jina la mtu ni muhimu sana. Jina lako ni muhimu zaidi. Yanapotajwa majina ya baadhi ya watu kuna kitu ambacho lazima kijnakuja katika akili yako.  Mfano likitajwa jina la MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE, moja kwa moja akili yako itajua kwamba huyu ni mkombozi wa Tanzania, baba wa taifa na raisi wa kwanza wa nchi hii.

SOMA ZAIDI; tatizo si rasilimali zilizopotea-7

Hii yote ni kutaka kuonesha ni kwa jinsi gani jina lilivyo na umuhimu mkubwa sana maishani mwako. Hii ndi o kusema kwamba kile ambacho unakifanya leo hii kitakuja kuwa na mchango mkubwa sana mbeleni. Watu watakuja kukumbuka wewe hapo kwa sababu ya kile ambacho unakifanya.  Watu watakukumbuka wa sababu ya alama ambayo utakuwa umeweka, ambayo inawagusa.
Je, wewe leo hii tukiwauliza watu watakukumbuka kwa jambo gani? Je, ni kitu gani ambacho umefanya ambacho kiwagusa wattu wengi sana? Je, unafiikiri miaka 100 ijayo watu watakaa waanze kuongelea nini juu yako? Ni kitu gani hicho? Kitafute kitu hiki ambacho dunia itakuwa inakaa na kuanza kushangaa kwa weredi wako wa kukifanya miaka 100 ijayo.
Tukatane kileleni.
NDIMI GODIUS RWEYONGEZA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X