TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA-64


Tatizo unataka kucheza peke yako uwanjani
Wachezaji wa mpira wa miguu wanatufundisha jambo jema sana ambalo tuunapaswa kulifahamu maishani. Kila wanapoingia uwanajani kwa pamoja wanashirikiana na kucheza mpira kwa pamoja. Huwa wanahakikisha kwamba wanapasiana mpira. Hakuna mchezaji wa mpira ambaye huwa anakaa na mpira peke yake muda wote ili yeye aonekane kwamba anajua sana zaidi ya wachezaji wengine.
Kitu kizuri zaidi ambacho huwa kinatokea uwanjani ni pale ambapo mchezaji mmoja anatolewa uwanjani ili aingie mwingine. Wachezaji wa mpira wa miguu huwa hawaachi kushirikiana naye kwa sababu tu eti hakuingia uwanjani mwanzoni. Tena huwa unakuta wanampokea kwa  upendo wa hali ya juu sana, akishaingia  tu anapewa mpira. Hii ni kutokana na ukweli kwamba wanategemea makubwa kutoka kwake muda wote. Hakuna mchezaji wa mpira ambaye anaonekana kwamba si wa muhimu. Wala hakuna mchezaji wa mpira ambaye hana umuhimu mkubwa sana anapokuwa uwanjani. Ndio maana hata Yule ambaye aliingia uwanjani baadae huwa annapewa mpira na kutegemewa kufunga goli. Mara nyingi sana huwa inatokea  na unakuta kwamba mchezaji aliyetokea nje anafunga goli na kuwanyanyua watu kwenye viti vyao.
Kwa kuwaangalia watu hawa [wachezaji wa mpira] tunapata kujifunza somo kubwa sana katika maisha yetu ya kila siku. Tunapata pia kujifunza somo kubwa katika bishara. Hii ndio kusema kwamba ili biashara yako iweze kuwa yenye mafanikio makubwa sana basi unahitaji kuwaajri watu, kushirikiana na watu na kuwa na umoja wa hali ya juu sana na timu yako ya uchezaji {timu ya biashara}. Hii ndio kusema kwamba tegemea watu wakusaidie kufunga hata pale wewe utakapokuwa umekabwa na watu kutoka timu ya upinzani. Waamini pia wale wale ambao hukuanza nao mwanzoni kwenye mchezo wako.
Mwisho unapasawa pia kuwa mfuatiliaji. Hata kama utakuwa umewaajiri watu na unafanya nao kazi, basi muda mwingi sana utumie katika kuhakikisha kwamba kazi ambazo umewapa zimefanyika katika kiwango ambacho wewe hapo unataka. Hii haimaanishi kwamba ukifuatilia kwa umakini  huwaamini, hapana, ila kuhakikisha kwamba kazi zako zimefanyika kama ambavyo ulikuwa unataka wewe zifanyike.
Ndimi,
GODIUS RWEYONGEZA
0755848391
songambele.smb@gmail.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X