TATIZO SI RASILIMALII ZILIZOPOTEA-59 Tatizo hutaki kuchoma meli moto


Kuna watu ambao wanapenda sana kufanikiwa ila bado hata vile vitu ambavyo vinawavuta kutoka kwenye mafaniko wanavipenda. Nikiona watu wa aina wanakuwa wananikumbusha juu ya hadithi ya ya fisi ambaye alichukua njia mbili mwisho wa siku akapasuka. Bila shaka na wahenga walikuwa wanafikiria mbali na walikuwa tayari wameona kitu cha maana kubwa sana pale walipokuja kusema kwamba njia mbili zilimshinda fisi.’
Hahahah! Lengo langu sio kumponda fisi leo. Hasha, ila nataka ujifunze kitu cha mubimu sana kutokana na huyu fisi ambaye hakuwa na  malengo wala mwelekeo. Fisih Huyu ambaye alikuwa akiyumbishwa na upepo.  Bila shaka yaliyomkuta fisi yanawakumba wengi sana kwenye kizazi cha sasa hivi.’
Yaani hii ndio kusema kwamba kwa sasa kuna watu wengi sana ambao wao wangependa kupata mafanikio ila kwa sababu bado wanageuka nyuma na kuona kwamba nyuma yao kuna meli zao zimewasubiri wanashindwa kuhakikisha kwamba wamesonga mbele. Yaani wanachukua njia mbili.
Njia ya mafanikio wanaipenda na njia ya kushindwa wanaipenda. Mwisho wa siku wanashindwa kusafiri njia moja na kuweza kuifikia mwisho.
Hawajui kwamba safari ya mafanikio inahitaji kuchoma meli moto, kiasi kwamba ukigeuka nyuma na kuona kwamba kuna moshi badala ya meli, basi utakazana kuhakikisha wkamba umeweza kufikia ushindi mkubwa sana.
Kama wewe unaweka akiba ila kila unapokutana na kitu kidogo tu unaitoa na kuitumia yote jua kwamba bado hujachoma meli moto kama ambavyo inatakiwa. Hivyo, rudi nyuma kidogo na kuhakikisha kwamba umechoma meli moto baada ya hapo uendelee na safari. Ndio unapaswa kurudi nyuma kwa ajili tu ya kuchoma meli moto wala sio jambo jingine.
Je, nitachomaje meli moto ili niendelee kuweka akiba kwa muda mrefu mpaka lengo litakapokuwa limetimia?
Asante sana mheshimiwa kwa swali lako jema sana. Ili uendelee kuweka akiba kwa muda mrefu sana kuna njia rahisi sana yaw ewe kuendelea kuweka akiba huku ukiwa na uhakika kwamba umechoma meli yako moto
>>>>kafungue akaunti ya mpesa, tigo pesa au airtel money leo hii ambayo utaanza kweka akiba yako. Katika kufungua akaunti hii hakikisha kwamba unamtafta mtu ambaye unamfahamu na mtu ambaye unamheshimu au kumwogopa. Mwambie lengo lako . mwambie kwamba sasa umefungua akaunti ambapo utakuwa unaweka pesa kwa kipindi bila kutoa. Katika kufungua akaunti hiyo hakikisha kwamba Yule mtu anashiriki katika kuweka nambari ya siri. Hii ndio kusema kwamba wewe utaweka nambari za siri mbili nay eye atamalizia mbili za mwisho. Bada ya hpo kila mmoja wenu atabaki na nambari zake bila kumambia mwingine.endelea kuweka akiba mpaka pale kiasi cha pesa ulichokuwa unahitaji kitakapokuwa kimekamilika. Hapo ndipo atakuruhusu wewe kuitoa na kukwambia nambari ya siri.

HAPO UTAKUWA UMECHOMA MELI MOTO KABISAAAAA!

>>>> Fungua akaunti ya benki ambayo hutakuja kuchukua atm card yake. Yaani unaiacha pale pale benki. Ifanye owe ya kuweka akiba tu sio kwa ajilil ya kutoa akiba.
Hii ndio kusema kwamba ukitaka kutoa pesa utatakiwa kuhakikisha wkamba umejaza fomu ya kuitoa na kupitia mlolongo mrefu sana.
HAPA UTAKUWA UMECHOMA MELI MOTOOO!!!
ANZA LEO!
CHOMA MELI MOTO SASA.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X