Hatua Sita Za Kujenga Maisha Ya Kuigwa.


Habari ya siku hii ya leo rafiki na ndugu msomaji wa Makala kutoka katika blogu hii ya SONGA MBELE. Imani yangu kwamba leo ni siku njema sana kwako na unaenda kuweka juhudi kubwa sana kuhakikisha kwamba umeweza kufikia mafanikio makubwa sana. Ndani ya siku hii ya leo tujifunze hatua sita ambazo zitatufanya sisi tuishi maisha makubwa sana. Maisha ambayo watu wengi sana watapenda wayaige, hali itakayopelekea wewe hapo kuwa mwalimu na kuanza kuwafundisha watu mbinu na kanuni hizi hapa ambazo utazitumia.
 Je, hatua hkzi sita ni zipi?
Ndio, hatua hizi hapa ni
1. KUWA MZALISHAJI
Kila mara hakikisha kwamba unakuwa mzalishaji bora. Unazalisha mawazo bora, zalisha mbinu bora za kukusaidia wewe, familia yako na jamii kiujumla. Usijiziuie kwa kile ambacho unakifanya. Tafuta kufanya kilicho bora kila wakati ili jamii iliyokuzunguka iweze kufaidika zaidi na kile kilicho ndani yako.

2. JENGA TIMU.
Kuna usemi unaosema kwamba “wewe ulizaliwa peke yako, hakikisha unaishi maisha kiasi kwamba utakapokufa unaacha jumuiya”. Hakikisha kila wakati unalenga katika kujenga jumuiya. Na jumuiya ya watu haijengwi kwa siku moja. Hasha, Bali jumuiya inaanza kwa kujenga uhusiano mzuri na mtu mmoja uliyenaye. Hii ndio kusema kwamba unapaswa kuhakikisha kwamba unaishi kwa falsafa ambayo haimwachi mtu jinsi alivyo. Ishi falsafa ambayo kila unapokutana na mtu mpya walau unaongeza thamani na haumwachi jinsi ulivyomkuta. Kwa jinsi hii utaweza kujenga jumuiya kubwa sana ya watu kila uendapo.

3. USISAHAU ULIPOTOKA.
hapa simaanishi kwamba kila wakati wewe unapaswa kukumbuka ya nyuma. Bali unapaswa kuhakikisha kwamba unakubali ulipo. Hii ndio kusema kwamba kama wewe umezaliwa barani Afrika usianze kusema kwamba bora ningezaliwa mbwa ulaya. Kwa kusema hivi utakuwa hujajikubali wewe mwenyewe. Lakini pia utakuwa unamaanisha kwamba wewe umezaliwa hapa kwa bahati mbaya sana. Kitu ambacho sio kweli. Hivyo. Hakikisha unakubali kwamba haupo hapo kwa bahati mbaya sana.

4. JIJENGE KIROHO
Umezaliwa, kwa bahati njema sana ukajikuta katika familia inayoamini juu ya misingi fulani ya kidini. Bila shaka na wewe umeendelea kwa kufuata misingi hii aua hata kama umeamua kufuata misingi yako. Hakikisha kwamba misingi hii hauipotezi.  Haileti maana kukuta kwamba mambo mazuri yanayotokana na imani yako hujayafanyia kazi. Itumie imani yako vizuri.

5. IFAHAMU KANUNI YA MBEGU
Hakuna mtu ambaye huwa anahangika kupanda mti wa matunda. Lakini ambacho huwa kinafanyika ni kwamba mkulima huwa anapanda mbegu. Kila anapopanda hutegemea mti kuota. Mkulima huwa anahakikisha kwamba anaweka mazingira bora kwa ajili ya ile mbegu kuota. Lakini mkulima haoteshi mbegu. Hii ndio kusema kwamba mkulima anahakikisha kwamba amefanya kazi zake kwa bidii na kadiri ya uwezo wake mengine Mungu huwa anamalizia.

6. JENGA MISINGI
hakikisha kwamba unajenga misingi bora sana. Jenga misingi ya maisha. Misingi yako itakwambia ni kitu gani unapaswa kufanya na ni kitu gani hupaswi kufanya. Kwa jinsi hii utakuwa katika sehemu nzuri sana ya wewe kukua na kutoyumbishwa na upepo utakaopita ili kukuyumbisha.

Haya ndio mambo ambayo unayahutaji kuyafahamu kwa ajikibya kujihakikishia kwamba unaweza kufikia hatua kubwa sana.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X