Hivi Ndivyo Vitu Vitatu (03) Ambavyo Watu Hudharau Sana.


Kuna vitu ambavyo huwa vinapendwa sana na watu wengi sana. Huku kukiwa na vingine havipendwi na kudharauliwa. Mfano unakuta vijana wengi sana wanapenda kuangalia mpira na kuhukumu wachezaji ambao wao (vijana) wanasema hawachezi vizuri japokuwa wao hawataki kuingia uwanjani kucheza. Na pengine mwingine ukimwambia aingie uwanjani acheze atakwambia mimi muda Wangu wa kucheza tayari umepita wakati wake. Je, na wewe umewahi kusema hivyo? Au umewahi kukutana na mtu wa aina hiyo?

Sasa ndani ya siku hii ya leo nimekuletea vitu vitatu vinavyodharauliwa sana nan watu. Je, vitu vyenyewe ni vipi?

1. WATU
Hivi ushawahi
 kugundua kwamba watu tunaowapenda zaidi ndio huwa tunawadharau zaidi! Hivi unajua kwamba wale tulio nao karibu huwa hatutumii muda mwingi kuongea nao? Unajua kwa nini? Hii ni kutokana na ukweli kwamba tunao, kwa wakati huo na tunachukulia kawaida tu! Tunaona kwamba hawa watu watakuwepo maisha yao yote. Ndio maana huwa hatuwapi kipaumbele. Bila shaka ndio maana wahenga wakasema “akujuaye hakuthamini”. Ndio maana unakuta una mtu karibu, badala ya kushirikiana na wewe mkaongea na kujijenga. Yeye anakuwa anachati na waleee wa mbali. Kwa sababu anajua si upo tu? Si upo tu muda mwingi.
Kama unataka kuwa bora sana katika suala zima la mahusiano hakikisha kwamba unawapa kipaumbele wale waliokuzunguka

2. MAARIFA
Kutokana na ile hali ya watu kupenda kujulikana kwamba wao wanajua. Basi, inakuwa vigumu, tena vigumu sana watu hawa kutafuta Maarifa mapya. Hivyo kujikuta kwamba wanaanza kufanya vitu kwa mazoea. Anafanya kwa sababu tu kitu ndivyo alivyokifanya na jana yake. Anafanya kwa sababu tu babu zake walikuwa wanafanya hivyo. Haki hii ndio inadidumiza ubunifu ulio ndani ya watu wengi sana. Hivyo kama wewe ni mmoja wao, jirekebishe. Biblia inasema “watu wanaangamia kwa kukosa maarifa”. Kwa nini uwe wewe unayeangamia bila ya kuwa na maarifa? Yatafute. Ni bora kununua kitabu kinachoonekana cha bei ghali, ila ukapata Maarifa yenye thamani mara milioni ya ile pesa uliyotoa.

3. MUDA
Kwa siku kila mtu ana masaa 24.  kumbe muda upo wa kutosha eti! Ndivyo wanavyojiambia wapumbavu. Wanafikiri wapo kwa ajili ya muda, ingawa muda upo kwa ajili yao. Wanafikiri wakipoteza SAA mkja watapata masaa 24 mengine zaidi. Kiukweli ninachoweza kukwambia ni kwamba “utumieni vizuri muda huu, maana ni kidogo sana na siku zijazo ni mbaya zaidi kama hutapangikia muda wako sasa”. Kama utaweza kuutumia vizuri muda wako utakuwa umeingia kwenye kundi la magwiji. Ni hayo tu Rafiki yangu.
Rukutane kesho aaubuhi na mapemaaa!


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X