Kila siku inapoanza tunaenda kujishughulisha na kazi au shughuli fulani. Hii ndio kusema kwamba kila mtu walau kwa siku kuna shughuli fulani ambayo yeye lazima aifanye. Hata kama ni ndogo kiasi gami lakini lazima ifanyike. Kinachotokea watu wengi wanajaribu kufanya kazi badala ya kufanya kazi haswa.
Matokeo yake ni kwamba kazi nyingi sana ambazo watu wanafanya zinakuwa hazijakamilika. Na zinakuwa hazina ubora.
Lakini miongoni mwa vitu vya muhimu sana ambavyo unahitaji kuvifahamu ni kuhakikisha kwamba haugusi, badala yake unafanya haswa. Hivyo hakikisha kwamba kila kitu ambacho unaruhusu mkono wako kugusa unakifanya haswa kwa asilimia 100. Yaani kwa ubora wa hali ya juu sana. Hata kama unafagia, fagia vyema kiasi kwamba hata siku moja ukipata likizo na usifagie watu waumie kwa sababu tu hujafagia.
Ninajua una uwezo wa kufanya hivyo,, anza leo na hakikisha kila unavhokigusa basi unakifanya kwa ubora wa hali ya juu sana.
Asante na kuwa na siku njema sana.