TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA-65 Tatizo hutaki kusema ndoto yako


Mara nyingi sana watu wanakuwa na ndoto ya kupiga hatua na kwenda mbele zaidi. Ila ndoto zao wanaogopa kuzitaja kwa watu wakiogopa maneno ya watu. Kama unaogopa kuongea ndoto zako mbele ya watu jua kwamba kuna kitu ambacho kinakosa kwenye ndoto zako. Kaa chini sasa na uhakikishe kwamba unazipitia tena ndoto zako. Maana kama wewe mwenyewe hazikupi motisha huwezi kupata ujasiri wa kuongea ndoto zako mbele ya watu. Hii ndio kusema kwamba huwezi kupata motisha ya kuzungumzia ndoto zako  basi hata wewe hutapata nguzvu ya kuziendeaa na kuzifanyia kazi.
KUNA UMUHIMU GANI WA MIMI KUONGELEA NDOTO ZANGU KWA WATU?
Kabla sijakwambia umuhimu wa wewe kuongelea ndoto zako kwa watu naomba nikukumbushe hadithi ya mwanajeshi wa kihispania aliyeenda jeshini na jeshi dogo kwa ajili ya kupigana na jeshi kubwa sana. Baaada ya kufika kwenye ardhi ya adui aliamua kuchoma moto meli zilizoleta wanajeshi wake. Huku wanajeshi wake wakishangaaa, alisimama na kuwambia maneno haya, “ mnanona meli ambavyo zinaungua”?  “hii imamaanisha kwamba hatuwezi kuondoka hapa mpaka tujihakikishie ushindi”. Alichokifanya mwanajeshi huyu kilikuwa ni kutangaza ndoto yake. Walitamgaza ndoto yake kwa wanajeshi wote ili waisikie na mwisho wa siku waanze kuifanyia kazi. Kilichoto0kea ni maajabu. Jeshi lake dogo sana liliweza kulipiga jeshi kubwa sana la adui.
Hii ndio kusema kwamba tukitangaza ndoto zetu kwa watu hata kama zitaonekana ni kubwa sana kiasi gani bado tutaaweza kuzikamilisha. Hii ni kutokana na ukweli kwamba

SOMA ZAIDI; TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA-59  tatizo hutaki kuchoma meli moto

#1. Hakuna ambaye anapenda awaambie watu kitu na mwisho wa siku ajikute kwamba kile kitu kimemshinda kukikamilisha. Hivyo ukiiwaambia watu utahakikisha kwamba unafanya chini juu kuhakikisha kwamba ndoto yako umeweza kuitimiza.
#2. Ukiwaambia watu ndoto zako utakutana na watu wambao ni sahihi  katika barabara ya kuiendea ndoto yako. Hii ndio kusema kwamba kama hutawaambia watu juu ya kile ambacho unacho ndani yako hata wale ambao wata kuwa tayari kwa ajili ya kuhakikiksha kwamba wanakusaidia hawatwaweza kujitokekza kwa sababau tuw hawajui kile ambacho wewe hapo unafikiria katika akili yako.
Hakikisha kwaba unasema ndoto ambazo wewe unaona kwamba unaweza kuwaabia watu ili kama wanakupa ushirikiano wao na wao wafanye hivyo, hata hivyo sio kila kitu lazima ukiongee kwa watu. Kuna vitu ambavyo utakaa navyo moyoni mwako kwa ajili yako. Na kuna vitu vingine ni siri kubwa sana, hivyo havipaswi kuongelewa tu hovyo hovyo kwa watu.
Hayo ndio mambo ya muuhimu sana ambayo unahitaji kuyafahamu na kuchukua hatua siku hii ya leo.
Ndimi rafiki yako wa karibu sana
KOCHA GODIUS RWEYONGEZA
($ongambele)

0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X