TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA-68 Tatizo hujawatumia watu wengine


Watu walio pembeni mwako kuna kitu kizuri sana ambacho wanakiona kwako ambacho wewe hapo huwezi kukiona. Kama utaweza kukijua vizuri kitu hiki kutoka kwa watu wengine basi utaweza kufaidika kwa hali ya juu sana. Hivi ushawahi kugundua kwamba mtoto mdogo sana akiwa ana kitu ambacho anataka kufanya anakuja kwa mzazi kuomba msaaada. Mfano mtoto atakuja kwa baba akisema hivi “baba naomba unisaidie kufunga makanda wangu”. Kumbe mtoto anajua kwamba kuna kitu ambacho yeye kama yeye hajui ila baba yake anakijua. Kwa sababu hiyo anakuja kwa mzazi wake kuomba msaada ili aweze kusaidiwa. Vivyo wewe kuna wakati utapasa kwendakwa watu kwa ajili ya kuomba msaada. Yaani utapaswa kwenda kwa watu ukiwaomba wakusaidie kufunga  mkanda wa suruali lako, ukiwaomba watu wakufunge vifungo vyako. Kwa kufanya hivi utaweza kufaidika na maarifa ,makubwa sana ambayo yanatokana na watu hao ambayo yatakuwezesha kusonga mbele zaidi na zaidi. Je, ni watu gani ambao unaeanda kuwaomba msaada kwa siku hi ya leo? Chukua hatu sasa.
Kumbuka kwamba kuna vitu ambavyo vimejificha katika kila kitu.  Hivyo si rahisi wewe kuona kila kitu ambacho kimejificha ndani ya kile kitu.  Kwa mfano kwa jinsi ambavyo unakiangalia kitu kimoja wewe ni tofauti na anavyokiangalia rafiki yako. chukulia jinsi unavyoiangalia mbegu wewe hapo ni tofauti na anavyoaingalia mtu mwingine. Wewe unaweza kuingalia mbegu kama mbegu ila mkulima akawana mtazamo wake wa tofauti na wewe hapo. Mkulima anaweza kuigalia mbegu hiyo na kuona mazao (mfano mahindi, maharage, n.k) wakati mmiliki wa mashine ya kusaga anaweza kuona unga mzuri kutoka katika mbegu hiyo hiyo. Hii ndio kusema kwamba katika kitu kimoja kuna vitu vingi sana ambavyo vimejificha. Na hivo unapaswa kuhakikisha kwamba vitu vingine ambavyo huvioni unaviangalia kwa watu wengine amb ao wamekuzunguka.
SOMA ZAIDI; MWANAMAHESABU WAKO NI NANI?
Ngoja nimalizie makala haya kwa kukuuliza maswali. Je, ukimwona jongoo unaona nini?  Basi kwa ufupi ni kwamba kuna mtu alishakaa na kuona treni kwenye jongoo. Unaona eeh! Hii ndio kusema kwamba yale ambayo huyaoni katika kitu Fulani watu wengine wanayaona. Sasa kazi ni kwako, hakikishaa kwamba na wewe unaona kitu ambacho kinaendana na kazi ambayo unaifanya katika kila kitu. Kama unafanya kilimo hakikisha kwamba ukimwona jongoo, unamwona kikilimo zaidi,
Kama wewe ni dereva hakikisahakwamba unamwona jongoo kiderev a zaidi
Kama wewe ni mwalimu hakikisha kwamba unamwona jongoo kiualimu zaidi.

Baada ya hapo tumia kile ambacho umejifunza kuwasaidia watu wen gine zaidi.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X