TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA-70 Tatizo ni hujaandika kile unachotegemea kutoka kwa watu


Je, ni mara ngapi umeaachia watu kazi na unakuta kwamba ile kazi uliyokuwa umewaachia  hawajaifanya? Je, ni mara ngapi kazi ambayo ulikuwa unategemea kuwa imefanyika umekuta hijafanyika? Je, unajua kwa nini?
Bila shaka hapa utaniambia kwamba watu ambao nawaaambia huwa hawanisikilizi. Badala yake wao huwa wanawafanya kazi zao ambazo wanapenda kufanya. Ngoja nikwambie kitu cha muhimu sana ambacho unahitaji kuhakikisha kwamba umekifahamu ili biashara na shughuli zako ziweze kukaa vizuri. Kitu hiki ni kwambwa watu wanasahahu sana kile ambacho unawaambia. Hii ndio kusema kwamba kama utaongea sana kwa kuwaaambia watu mwisho wa siku utakuta kwamba wamesahau kile ambacho uliwaambia. Hivyo haupaswi kuwa mtu wa maneno mengi sana kila siku ukiwaambia watu wako fanya hiki, acha hicho. Kuna njia rahisi sana ya wewe kuweza kuwaambia watu wafanye kazi kwa ubora wa hali ya juu sana. Njia hii ni kuandika maneno mafupi sana ambayo yanawaaambia wafanyakazi wako kitu gani ambcho unategemea kutoka kwao. Hakikisha kwamba unaandika maneno mafupi ambayo hata mtoto wa miaka sita akiyasoma atayaelewa vizuri tu. Wape wafanyakazi wako karatasi yenye maneno hayo. Pale watakapokuwa wakiyasoma watakuwa wakikumbuka kile ambacho wanapawa kufanya. Hali hii itakupunguzia kiasi cha kuwa unawapigia simu mara kwa mara. Jambo hili sio tu kwammba uwaambie wafanyakazi wako kitu gani ambacho unategemea kutoka kwao. Bali waambie watu wote ambao  unakutana nao maishani mwako. Waambie ni kitu gani ambacho unategemea kutoka kwao kwa maandishi. Waaambie kwamba unategemea kufikia tarehe Fulani unategemea wawe wamefanya kazi na kuikamlisha. Waambie juu ya majukumu yao ya siku, wiki na majukumu yao ya mwezi. Kwa hali hii utakuwa katika hali hii utakuwa umepunguza majukumu madogo ambayo yangeweza kufanywa na watu wengine ila yanafanywa na wewe hapo.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X