Watu wengi sana wanahairisha kuishi kila kunapokucha. Anasema kwamba atafanya kazi fulani kesho. Ataishi maisha fulani kesho,
Ataanza kula vizuri kesho akipata kazi nzuri.
Ataanza kuongea na watu vizuri kesho….orodha ya namna hii ni kubwa kiasi kwamba siwezi kuimaliza hapa.
Je, na wewe mmoja wapo?
Kwanza kabisa naomba tufahamu kwamba kesho sio siku.(Rweyongeza, 2017)
Pili tunapaswa kufahamu kwamba muda wa kuishi vizuri ni sasa.
Kama tutaishi vizuri Sasa sio tu kwamba tutakuwa tumefanya tunayopaswa kufanya ndani ya siku hii ya leo bali pia tutakuwa tumeitengeneza kesho bora.
Anza kuishi Sasa.
Kama sio Sasa lini?
Kama sio wewe nani?(Rweyongeza, 2017)
Vitabu muhimu vitakavyokusaidia kuielewa mada hii kwa undani
1. KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI (tsh 10,000/-) by Godius Rweyongeza
2. BARABARA YA MAFANIKIO (6,000/-) by Edius Katamugora
TUKUTANE KWENYE MEZA YA WANAMAFANIKIO.
Tukutane kwenye mzunguko wa wanamafanikio.
©songambeleblog_2017
Ndimi,
Kocha Godius Rweyongeza
($ongambele)
0755848391
songambele.smb@gmail.com