TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA -80 Tatizo unafukuza swala wawili


Kuna msemo wa Kiswahili ambao unasema kwamba “mshika mbili moja humponyoka”. Bila shaka wahenga waliosema maneno haya walikuwa wanawalenga watu ambao katika maisha yao wanalenga sehemu kubwa sana za kimafanikio lakini bado hata yale mambo ammbayo yanawatoa kwenye mafanikio bado wanayataka. Watu ambao wanapenda kuwa na maisha makubwa sana kiuchumi, kijamii na kimahusiano lakini bado wanafanya vitendo ambavyo vinawazuia wao kuwa hivyo. Kumbe ndio maana watu wengine wakasisitiza kwa kusema kwamba “mtaka yote kwa pupa hukosa yote”.
Jambo moja la msingi sana ambalo unaaweza kufanya katika maisha yako ni kuhakikisha kwamba  unajua wapi unaenda. Baada ya hapo rahisisha mambo. Badala ya kutaka kufanya hiki na kugusa kile, kwenda kulia na kushoto wewe amua kwamba utafanya kitu kimoja ambacho kitaongeza thamani kubwa sana kwenye maisha yako.  Kiasi kwamba watu wakiulizwa kitu kimoja tu ambacho kinakuhusu wewe hapo basi wawe wanajua wanaongelea nini juu yako.
Moja kati ya wanafalsafa maarufu sana hapa duniani ambaye ni Confusius aliwahi kusema “mwanadamu anayefukuza swala wawili hawezi kumakamata hata mmoja”. Alikuwa sahihi.
Sasa wewe jiulize ni kwa muda gani sasa umekuwa ukifukuza swala wawili.  Kila siku unapang a kumfukuza swala Fulani kwa kupangilia ratiba yako ya siku lakini katikati ya siku unakutana kitu kingine cha kufanya na unasahahau ratiba yako ya awali. UNAFUKUZA SWALA WAWILI
Mwanzoni mwa mwaka huu uliweka lengo na kuhakikisha kwamba umeiliandika lakini kwa sasa, kadri  mpaka sasa umelipoteza na hukumbuki wapi  uliliandika. Kitu kingine ni kwamba umeanza kuishi malengo ambayo hata ulikuwa hujayapanga. HAPO UNAFUKUZA SWALA WAWILI

Watu waliofanikiwa sana katika maisha yao ni watu ambao wanafukuza swala mmoja. Wana picha haswa ya swala ambaye wanamhitaji, rangi ya swala, na ukubwa wa swala. Hawajaishia hapo tu wanajua hata wakimchinja watapata kilo ngapi? Watamtumiaje baada kumshika na bado wameeleza vitu ambavyo vinaweza kuwakwamisha kumkamata swala wao. Je,wewe unaweza kuniambia swala gani unamfukuza? Tafakari chukua hatua!


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X