TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA -81 tatizo haujawa mwekezaji


.

Hivi ushawahi kujiuliza ni kitu gani kampuni inahitaji ili kukua?
Kama hujawahi kujiuliza swali kama hili hapa, ebu kaa chini na ujaribu kujiuliza swali hili hapa muhimu sana. Utagundua kwamba ili ukue unahitaji kuwa na watu. Ni watu ndio ambao wanakubeba. Ni watu wenye uwezo wa kukusimamisha. Ni watu wenye uwezo wa kukuangusha. Je, unajua hilo? Kwa hiyo hakikisha kwamba unawekeza katika watu.

Sasa nitawekezaje katika watu?
Hili ni swali la muhimu sana ambalo unaweza kuwa unajiuliza asubuhi ya leo?
Usihofu Rafiki yangu.
Wekeza kwa watu kwa kuwapa maarifa. Ndio maarifa. Kuna mtu mmoja aliwahi kusema kwamba “njia nzuri ya kumfanya mtu asikuombe samaki ni kumfundisha kuvua samaki maisha yake yote”. Bila shaka aliyesema maneno hayo alikuwa hajaenda mbali sana na Mimi. Alikuwa anapenda watu wapewe maarifa. Ukimfundisha mtu kuvua samaki unakuwa umempa maarifa. Kumbe kitu kikubwa unachoweza kuwekeza kwa watu ni maarifa. Lakini mimi binafsi sipend uishie tu kufundisha watu maarifa ya kuvua samaki. Sio kwamba nampinga yule aliyesema njia nzuri ya kumfanya mtu asikuombe samaki maisha yeke yote mfundishe kuvua samaki. Kidogo mimi hii sentensi naiangalia kwa jicho langu la dhahabu na nimeona sentensi yenye maana bora zaidi ni “njia nzuri ya kumfanya mtu asikuombe samaki, mfundishe jinsi ya kumiliki bwawa la samaki”. 😁😁  umegundua nini hapo?
Mmiliki wa bwawa la samaki ni tofauti kabisaaa! Na mvuvi. Kwenye bwawa moja la samaki wanaweza kuja wavuvi wa samaki kumi. Na wote wakamlipa mmiliki wa bwawa la samaki. Unaona Sasa. Kwa hiyo njia nzuri ya wewe kuondoka kwenye umaskini sio tu kujua kuvua samaki. Unaweza kuwa unajua kuvua samaki lakini mwenye bwawa akasema leo sitaki uvue samaki kwenye bwawa langu. Njia nzuri ni kumiliki bwawa. Kwa hiyo wafundishe pia watu jinsi ya kumiliki mabwawa ha samaki.

Kumfundisha mtu kuvua samaki ni sawa na kumwelekeza mtu jinsi ya kutengeneza asali bila ya kujua jinsi ya kutengeneza mzinga.

Asante sana Rafiki yangu


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X