Kuna vitu ambavyo kwa kuviangalia katika maisha huwa vinaonekana vibaya ila kiukweli ndani yake hazina kubwa sana. Kwa kuuangalia udongo hakuna ambaye anaweza kusema kwamba udogo unaweza kutoa mti wenye matunda matamu sana. Maana unakuta udongo ni mchafu sana kiasi kwamba kama wewe ni mtanashati huwezi hata kupenda mtu yeyote Yule akugusishe udongo huo.
Lakini pia kwa kuuangalia udongo hata hakuna mtu ambaye anaweza kukwambia kwamba ndani yake unaweza kupata madini yenye thamani kubwa sana hapa duniani. Kiukweli kwa sababu tu ya uchafu wa udongo kama mtu angeleta maji na udongo na kukuuliza, “niambie ni wapi unategemea tutakuta madini yenye thamani kubwa sana”’ kwa haraka tu kwa sababu ya uang’avu wa maji na usafi wake, basi utasema ndani ya maji ndipo kuna madini yenye thamani kubwa sana. Lakini hali hata haiko hivyo. Hapo ndipo nakumbuka ule usemi wa wana falsafa wanaosema kwamba “uzuri wa kitu haupo kwa kitu chenyewe bali upo kwa mtazamaji”.
Siku zote vitu vichafu, vitu ambavyo hata vyenyewe havingai ndivyo huzalisha vitu vinavyongaa.
Ni maajabu kuona tupa haina makali lakini inanoa kisu chenye makali.
Ni maajabu pia kuona dawa ya viatu (kiwi) na weusi wake wote inang’arisha kiatu na kumfanya mtu apendeze.
Nia maajabu pia kuona kwamba sabuni inatumika kusafisha vyombo na kuvitakatisha.
Maajabu mengine ni pale unaposhuhudia mbegu inatengeneza meli (mbegu- miti-mbao-meli). hahahah
Mpaka hapo bila shaka utakuwa unajiuliza hivi SONGA MBELE leo amekuwaje, mbona anataja taja vitu ambavyo mimi sioni uhalisia wake katika maisha. Ebu subiri kidogo rafiki yangu tuzidi kusonga mbele. Mambo mazuri sana bado yanakuja.
Wewe hapo unapaswa kufahamu kwamba kuna kitu ambacho kimo ndani yako ambacho hata kinaonekana kwamba hakina umuhimu. Yaani kinaonekana kama udongo. Ni kichafu kiasi kwamba hata ukikiweka kwenye maji kukiosha hakiwezi kutakata mara moja. Lakini kama utakigundua kitu hiki na kuhakikisha kwamba umekifanyia kazi kitu hiki. Hakika wewe utakuwa mtu mkubwa sana. Kitu chenyewe ni kipaji chako. Je, una tupa ndani yako? Itumie kunolea visu kuanzia sasa hivi? Je, una udongo mchafu ndani yako? Panda mwembe, na siku zote watu watakuja kuvuna maembe karne na karne. Je, una kiwi ndani yako? Itumie kung’arisha kiatu, utakapopita watu watakusifia umependeza leo.
Una nini ndani yako? Una nini wewe?
JIPATIE KTABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI leo ili uweze kugundua kipaji chako ni kipi. Kitabu hiki pia kitakuelekeza jinsi ambavyo unaweza kugundua kipaji cha Yule umpendaye (rafiki, mwanao, mke au mme).
Amka 2018
Kipenga kimepulizwa2018
#KUTOKA_SIFURI_MPAKA_KILELENI