TATIZO SI RASILIMALI ZLIZOPOTEA-79 tatizo hujataka kuwa Thomaso


Moja kati ya watu ambao huwa wanazungumziwa sana kwa kutokana na kupenda kuhakikisha na kuuliza kwao ni Thomaso. Thomaso ninayemzungumzia hapa ni yule aliyeelezwa kwenye Kitabu cha Yohana 20:19-29 Imeandikwa hivi katika biblia “ikawa jioni siku ile ya kwanza ya juma pale walipokuwapo wanafunzi, milango imefungwa kwa hofu ya wahahudi, akaja Yesu, akasimama katikati, akawaambia, Amani ….”
“walakini mmoja wa wale tenashara, Thomaso, aitwaye pacha hakuwako pamoja nao alipokuja Yesu”. Basi wanafunzk wengine wakawambia, tumemwona Bwana. Akwaambia, Mimi nisipoziona mikononi mwake kovu za misumari na kutia kidole changu mahali pa misumari, na kutia mkono Wangu katika ubavu wake, mimi sisadiki hata kidogo”.

Binafsi namwona Thomaso kama jasiri mkubwa sana. Hii ni kutokana na ukweli kwamba watu wengi kwa sasa wanajitolea kukubali na kupokea kila kitu. Ila hawakai na kuchakata na kuangalia kipi kinafanya kazi na kipi hakifanyi kazi.
Hawataki kuuliza na kuhoji kwa undani zaidi ili kupata majibu yaliyokamilika. Uthomaso unahitajika katika zama hizi za taarifa.
Unahitaji kuhoji kwa nini uangalie movie fulani na kwa nini usiutumie muda huo kufanya kitu kingine?
Kwa nini unasoma Kitabu fulani na sio kingine?
Kwa nini mtu akikupigia simu unaharakisha kupokea?
Kwa nini ukiamka asubuhi kitu cha kwanza unashika simu?

Huu ndio Uthomaso unaopaswa kuwa nao!

Naomba nikutakie siku njema sana.

TUKUTANE KWENYE MEZA YA WANAMAFANIKIO.

Tukutane kwenye mzunguko wa wanamafanikio.

©songambeleblog_2017

Ndimi,
Kocha Godius Rweyongeza
($ongambele)
0755848391
songambele.smb@gmail.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X