TATIZO SI RASILIMALLI ZILIZOPOTEA-68 Tatizo hujajua kwamba hujuii kila kitu


Katika zama hizi kuna taarifa nyingi sana. Taarifa hizi zinatujia kwa njia tofauti tofauti sana katika maisha yetu. Taarifa hizi zinzaweza kukujia kupitia kwa watu ambao wamekuzunguka. Vitu unavvyokutana navyo, vikwazo vinavyokuzuia na vingine vingi. Hata hivyo kama hujajipanga kuzitafuta taarifa hizi  hapa huwezi kuzipata. Hii ndio kusema kwamba kama bado hujakubali kwamba hujui ili uweze kujifunza maarifa haya kutoka wa watu wengine huwezi kuyapata. Siku zote maarifa yanafuata mkondo, kama ambavyo maji yanafuata mkondo. Hii ndio kusema kwamba maarifa nayo yanatoka sehemu yenye kilima na kuja sehemu  ya bondeni (soma zaidi katika kitabu cha kutoka SIFURI MPAKA KILELENI).  Hivyo kama hutakubali kwamba hujui kwa hakika huwezi kupata hayo maarifa kutoka katika vyanzo tajwa hapo juu.  Kwa hiyo muda mwingine lazima ukubali  kwamba kuna maarifa ambayo unahitaji kuyapata kutoka kwa watu wengine. Chukulia kwamba umeenda katika mji ambapo unaenda kukutana na watu muhimu katika hoteli. Umeshuka katika uwanja wa ndege na hujui wapi utaelekea.  Utafanyaje? Lazima utatafuta watu wa kuuliza. Na utaenda mbali zaidi kwa kuhakikisha kwamba unatafuta mtu wa tax wa kukuwahisha kwenye hoteli husika. Kumbe hapo utakuwa umekubalil kwamba kuna kitu ambacho hujui na kukaribisha watu ambao wanajua zaidi ya wewe waweze kukushirikisha maarifa yao. Kama hutakubali kupokea maarifa kutoka kwa watu watu wenyewe hawatakuwa tayari kuja karibu yako. Maana watajiona kwamba si watu wa muhimu na hawafai. Kwa sababu hiyo mwisho wa siku utakuwa unazidi kupoteza maarifa mengi sana.
Kwa hiyo unapaswa kuhakikisha unfahamu kwamba maarifa  na rasilimali sio tu zile ambazo zinachimbwa katika ardhi. Hasha, maarifa  mengi zaidi yanachimbwa  katika vichwa vya watu.  Maarifa mengine zaidi yanachimbwa katika vitabu na vyanzo vingine vya maarifa.

Hakikisha unazitumia rasilimali hizi muhimu sana kila wakati na kila sehemu utakapokuwa ukienda.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X