Hawa Ndio Watu Watano (05) Ambao Unapaswa Kuwasikiliza


Habari ya siku hii ya leo Rafiki na ndugu msomaji wa blogu ya SONGA MBELE. Karibuni sana katika makala haya ya ya siku hii ya leo.

Kwa sasa tunaishi katika dunia ambayo ina kila aina ya kelele. Kila mtu anaongea, kila wakati. Kelele kutokea kila kona hazitupi muda wa wa kukaa kidogo na kusikiliza.  Tupo katika dunia ambapo tunakua kila siku. Na kukua huku si kuongezeka kwa kimo tu, bali hata kwa kuongeza maarifa. Katika hali ya kawaida maarifa yanakuja kwa kujifunza. Huwezi kujifunza huku ukiwa unapiga kelele. Unaweza kujifunza vizuri kama utakaa chini na kusikiliza. Sasa niwasikilize akina nani?

1. WASIKILIZE WATEJA
Earl Nightngale aliwahi kusema kwamba pesa yote unayoihitaji iko mikononi mwa watu. Hivyo ni juu yako kukaa chini ma kuwasikiliza watu ambao wanakuja katika biashara yako. Au kifupi wasikilize watu ambao unawahudumia katika biashara yako. Watu hawa unaweza kuwa unawaita majina mbali mbali kulingana na eneo ulilopo mfano kama huduma unayitoa ni ya hospitalini basi watu hawa utawaita wagojwa, kama huduma unayotoa ni ya shule utawaita wanafunzi, kama huduma unayitoa ni ya kusafirisha watu basi utawaita abiria. Vyovote vile utakavyowaita lakini neno moja kuu kwa watu wote ni WATEJA. Wasikilize hawa.

2. WASIKILIZE WATU WALIOPIGA HATUA ZAIDI YAKO
Unafanya nini? Kazi yako ni ipi? Je, kuna watu ambao wamepiga hatua katika kile unachokifanya? Kwa vyovyote vile lazima wapo. Unajua kwa nini wamekuzidi? Ni kwa sababu tu wana kitu wanakuzidi ambacho wewe hapo hukijui. Basi kuwa tayari kukaa chini kwenye miguu yao na uwasikilize. Hawa wana taarifa muhimu sana ambazo zitakuwezesha wewe hapo kuweza kupiga hatua kubwa sana.
Sasa kaa chini, orodhesha orodha ya watu watano ambao wamepiga hatua sana zaidi yako! Tafuta namba zao na omba kukutana nao ili ukae chini uwasikilize.

Soma zaidi; Jinsi Ya Kuongeza Ufanisi Kazini

3. WASIKILIZE WATAALAMU
Katika maeneo mbali mbali kuna wataalamu wa kila aina. Kama wewe ni mkulima, basi jua kwamba kuna wataalamu kibao unaoweza kuwasikiliza kwenye kile unachofanya. Kama wewe unapata shida ya mahesabu basi jua kuna wahasibu wanaweza kukusaidia juu ya hilo. Hawa ndio watu unaopaswa kuwasikiliza. Ngoja nikuulize swali, gari lako likiharibika huwa unafanyaje? Bila shaka utaniambia huwa nalipeleka gereji kwa fundi. Sawa. Ngoja nikuulize swali jingine ukiumwa unafanyaje? Bila shaka jibu lako nitaenda hospitali kwa daktari. Unajua fundi na daktari ni akina nani? Kama ulikuwa hujui hwa ndio wataalamu! Na ukifika hospitali  kama suala lako linahitaji uangalizi wa hali ya juu watakuambia nenda kwa daktari bingwa. Hii maana yake ni nini? maana yake unaenda kwa mtaalamu aliyebobea zaidi. Basi kama unaweza kufanya hivyo unapoumwa, basi Fanya hivyo pia sasa.

4. WASIKILIZE UNAOWAPENDA
Kaa chini umsikilize mpendwa wako, kaa chini usikilize mke/mme wako. Kaa chini uwasikilize watoto wako. Hawa ni watu ambao wako karibu sana na wewe. Ukiweza kukaa chini na kuwasikiliza kila siku basi jua kwamba utafaidika sana.

5. SIKILIZA VITABU VILIVYOSOMWA.
Kuna mtu mmoja aliwahi kusema kwamba muda ambao kwa sasa watu wananautumia kwenye safari (akiwa amekaa kwenye kochi) ni mara sawa na muda ambao ungemchukua mtu huyo huyo kupata shahada za uzamivu nne kipindi chote cha maisha yao. Kumbe unaweza kuutumia vizuri sana muda huu kujiendeleza binafsi. Unaweza kuutumia muda huu kusikiliza vitabu vilivyosomwa. Muda huu ni mkubwa sana kwa mwaka kiasi kwamba Brian Trancy anasema muda huu kwa mwaka mzima ni sawa na muhura mzima wa chuo (semester). Hivyo kama utautumia vizuri sana kwa miaka mitatu ijayo utakuwa na shahada ya kitu kile ambacho unajifunza kwa sasa.
Piga hatua endelea mbele. Sikiliza.

Ikumbukwe kusikiliza nilikodokeza hapa sio kule kukaa kwenye TV na kuanza kuangalia movie. Hasha! Au kusikiliza kukiwa na makelele kibao ya watu. Bali muda mwingi sana kunahitaji utulivu na umakini wa hali juu sana.


2 responses to “Hawa Ndio Watu Watano (05) Ambao Unapaswa Kuwasikiliza”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X