Hii Ndio Sifa Unayopaswa Kuiepuka


Hapa duniani kuna watu wenye sifa na mbali mbali. Sifa hizi zinaweza kuwa zinatokana na kazi ambayo mtu anafanya, sifa hii pia inaweza kuwa inatokana na cheo cha mtu. Pengine sifa ya mtu inaweza kuwa inatokana na marafiki ambao ameshikana nao. Lakini ukweli ni kwamba walau kila mtu ana sifa fulani.

Mwalimu wangu wa kiswahili alinifunifundisha kwamba ukisema kitu ni kibaya na yenyewe ni sifa. Lakini pia ukisema kitu fulani ni Kizuri nayo pia ni sifa. Kumbe sifa sio lazima iwe kama ambavyo unaifikiria Bali hata wengine wanavyofikiria.

Mbali na kwamba sifa zinaweza kuwa za aina nyingi sana na za aina nyingi sana. Kuna sifa ambazo hata huhitaji kuwa nazo. Leo hii nakudadafulia sifa mijawapo.
Na sifa hii ni moja tu. Ndio, ni sifa ya kibao.

Kibao ni sehemu yenye maandishi kinachokuelekeza kwenda sehemu fulani ila chenyewe hakijawahi kwenda.

Hahah! Bila shaka maishani mwako umewahi kukutana na vibao vingi sana.
Mara utakuta kibao kimeandikwa SHULE YA MSINGI MTAKUJA 1km ahead. Kibao chenyewe hakipajui!!!

Au utakuta kibao kimeandikwa NMB BANK (100m) huku kikikuonesha sehemu ilipo benki. Lakini kiulize unapafahmu penyewe ilipo hiyo benki. Hata hakijwahi kupaona.

Kumbe na wewe unapaswa kuiepuka sifa kama hii hapa. Yaani, sifa ya kuelekeza watu waende sehemu fulani ila wewe huendi au hujawahi kwenda.
Kuna watu huwa wanaishi kwa kusema “ninayosema fuata, ila nifanyayo usiige”. Sichelei kuwaita vibao maana wanaelekeza pa kwenda wakati wao hawaendi huko.

JAMBO LA KUZINGATIA SIKU YA LEO!
Usiishie tu kunyoosha kidole,
Usiishie tu kuagiza Fanya hiki, acha hicho, acha kile. Badala yake ingia uwanjani na wewe cheza mziki.
Nenda unaponesha badala ya kuonyesha tu kwa kidole.

Ulikuwa nami,
Godius Rweyongeza


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X