Sauti Tano Ambazo Hupaswi Kuzisikiliza Kamwe


Habari, baada ya jana kuzungumzia na kudadafua kwa undani juu ya watu watano ambao unapaswa kuwasikiliza. Leo hii ninaenda  kudadafua watu watano ambao kamwe hupaswi kuwasikiliza. Najua unajiuliza, inakuwaje anasema nisiwasikilize baadhi ya watu wakati jana alisisitiza sana juu ya Mimi kusikiliza?
Usihofu, ni kweli ni muhimu sana kusikiliza ila kuna sauti zinazoweza kukupoteza kama utaendelea kuzisikiliza. Kuna sauti zitakuangusha au pengine tunaweza kusema sauti hizi ni kelele. Basi naomba uzifahamu sauti hizi hapa;

Soma zaidi hapa;  Hawa Ndio Watu Watano Unaopaswa Kuwasikiliza
1. Sauti ambayo inalalamika na kuona ubaya katika kila kitu. Sauti hii si ya kusikiliza hata kidogo.

2. Usisikilize sauti inayosema mtu fulani, yupo nchi fulani ndie anayehusika na maisha yako. Fahamu kushinda na kwenda hatua ya ziada maishani mwako ni wajibu wako.

Soma Zaidi; Acha Kulalamika

3. Kuna sauti inawaongelea watu wengine, kuna sauti inasengenya watu wengine. Acha kuisikiliza sauti hii. Sauti hii kila wakati inawafuatilia watu wengine mutandaoni. Inakutaka na wewe uifuate.  Wewe ndiwe unahusika na maisha yako. Ukishinda ni juu yako, ukishindwa ni juu yako.

4. Acha kuisikiliza sauti inayokudogosha na kukuweka chini hata kama ni kwa sekunde moja. Hii sauti haipaswi kupewa kipaumbele hata kidogo.

5. Usimsikilize mtu aliyeshindwa katika kitu fulani na anakwambia haiwezekani. Kwa hakika mtu huyo si wa kusikikiza hata kidogo.

Hawa ndio watu watano ambao kamwe hupaswi kuwasikiliza maishani mwako. Wajue watu hawa, na hakikisha kila wakati unasikiliza sauti njema kama ambavyo imeelezwa kwenye makala ya jana.

Tukutane siku nyingine hapa hapa safuni!
Ulikuwa nami
Godius Rweyongeza
Jipatie  sasa nakala ya vitabu vyangu, TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA na KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI kwa pamoja kwa bei ya sh. 14,000tu badala ya sh. 20,000.
Tuma pesa kwenda nambari 0755848391 jina GODIUS RWEYONGEZA
baada ya hapo nitumie ujumbe wa njia ambayo ungependa nikutumie vitabu hivi, inaweza kuwa wasap, telegram au email.
Karibu sana.
Bei ya kitabu kimoja kimoja
1. TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA (6,000)
2. KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI (8,000).
bei hizi ni kwa siku chache tu baada ya hapo kila kitabu kitakuwa kinapatikana kwa sh. 10,000

KUJIUNGA NA KUNDI LA HAZINA YETU TANZANIA🇹🇿🇹🇿 BONYEZA HAPA

Kupata makala maalum kwa watu maalumu kila wiki bonyeza hapa


One response to “Sauti Tano Ambazo Hupaswi Kuzisikiliza Kamwe”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X