TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA-107 tatizo hutaki kujifunza


Moja kati ya jambo ambalo linaaminiwa sana na watanzania ni ule msemo wa ukitaka kumficha mwafrika kitu, basi kiandike katika kitabu. Binafsi msemo huu ninaenda kinyume chake kila siku. Ila kuna watu wengi sana ambao wanaukumbatia kila mara na kila ninappongea nao basi kisingizio chao ni kwamba waafrika huwa hatusomi vitabu. Waafrika huwa hamsomi vitabu? Wewe na nani? Yaani mtu anataka TATIZO lake alifanye liwe la jumuiya na bara zima. Kwamba yeye hasomi vitabu basi ni waafrika wote. Kama wewe husomi vitabu basi usiseme waafrika hatusomi vitabu ili kuonekana kwamba mko wengi, sema sisomi.

Ila kama unahitaji kupiga hatua na kuhakikisha kwamba unaenda hatua ya ziada katika maisha yako basi nakushirikisha vitu viwili muhimu sana ambavyo unavihitaji. Moja unahitaji maarifa, na pili unahitaji ujuzi. Vitu hivi vyote ili uweze kuvipata vizuri sana, lazima uwe tayari kujifunza.

Kujifunza ndio ufunguo wa mafanikio. Kutakuonesha fursa pale unapoona hakuna fursa. Kutakukutanisha na watu ambao wako mbali, kutakuonesha njia pale unapoona kuna miamba. Kutakuinua pale watu wanapoona unaanguka, kutakupaisha wakati watu wengine wanatembea.

Na mbinu nzuri sana ya kujifunza ni
1. kusoma vitabu.
“Tone la wino linaweza kufanya mamilioni ya watu kufikiri”, alisema Gordon Brion Noel. Kusoma kutaifanya akili yako ifikiri na kufikiri. Kusoma kutaifanya akili yako iangalie dunia sio kama ambavyo akili inahitaji kuiona, bali kama ambavyo dunia inaenda. Kusoma ni ufunguo wa fursa. Kwa hiyo wewe unapaswa kuwa mwanafunzi wa kudumu. Kila siku unatafuta maarifa mapya.

2. Kuhudhuria semina.
Sehemu nyingi sana kuna semina mbali mbali zinatolewa kila siku, kila wiki, kila mwezi. Unaweza kuhudhuria semina hizi ili uweze kupata maarifa mapya. Maarifa haya yapo kwa ajili yako. Ni juu yako kuwa tayari kuyapokea, maana kama.mwanafunzi hayupo tayari siku zote hawezi kumwona mwalimu hivyo utayari wako ndio utakuonesha waalimu wako wapi.

Asante sana

Ndimi,
Godius Rweyongeza
($ongambele)
0755848391
www.songambeleblog.blogspot.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X