TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA-108 tatizo hujajua kwamba hauzuiliki


Nenda unapotaka kwenda, fanya unachotaka kufanya unaweza kuwa unachotaka kuwa” zig ziglar.

Maisha ni kuchagua, unaweza kuchagua kuwa bingwa au kufeli. Ni juu yako. Ili uweze kufika unapotaka unapaswa kufahamu kwamba kuna vitu vikuu vitatu ambayo unavihitaji. Vitu ambavyo vitaweza kukuinua wewe hapo na kukufikisha unapotaka kwenda. Maana kila mtu huwa anapanga kushinda hata kama hajaandika chini, lakini washindi ni wachache sana. Hii ni kutokana na ukweli kwamba si wote wameweza kugundua siri ambazo zimeshirikishwa katika makala haya. Unaweza kwenda unapotaka kwenda maishani. Unaweza kuwa unachotaka maishani mwako lakini hapa kuna vitu vya msingi sana ambavyo sharti uvifuate;

1. Malengo.
Malengo ni jicho la kukuonesha Kile ambacho wengine hawawezi kuona. Kutoka sehemu moja kwenda nyingine basi malengo ni muhimu sana, sana.

Hivi ni kweli malengo yanafanya kazi?
Ndio malengo yanafanya kazi tena sana. Moja kati ya mifano mizuri sana ya watu ambao huwa wananipa hamasa kufikia malengo makubwa sana ni wajapani. Miaka ya 1950-1959 viongozi wa serikali, wafanyabiashara, wajasiliamali, na watu wote wenye mapenzi mema na taifa hilo waliweka lengo. “ebu tuwe taifa nambari moja hapa duniani katika kuzalisha bidhaa za nguo ndani ya miaka 10″. Lengo lao liliweza kutimia.

Miaka ya 60 wakaweka lengo jingine “ebu tuwe nambari moja duniani katika kuzalisha bidhaa za chuma”. Waliweza.

Miaka ya 70 wkaweka lengo jingine, “ebu tuwe nambari moja hapa duniani katika kuzalisha vifaa vya moto, mfano magari, pikipiki, n.k leo hii wewe ni shuhuda juu ya makampuni ya kijapani yanayofanya vizuri sana kwenye sekta hii. Ikiwemo kampuni ya Honda, Toyota, kutaja ila chache.

Miaka ya 80 wajapani waliweka lengo jingine. Sasa na tuwe nambari moja katika uzalishaji wa bidhaa za kieletroniki, makampuni ya kijapani yalianza kutengeneza simu na kompyuta kwa kiwango cha juu sana. Na lengo lao liliweza kutimia.

 Bila Shaka wewe utakuwa mmoja wa watu wanaoifahamu kampuni kubwa sana ya kieletroninki ya SONNY.

Kumbe malengo yanafanya kazi, iwe ni ya mtu binafasi, familia, kampuni, ushirika, wilaya, mkoa au Taifa.  Malengo yanafanya kazi. Sasa jiulize malengo yako ndani ya mwaka 2018 ni yapi? Unaenda wapi? Kwa nini unaenda huko? Kitu gani kinakusukuma kwenda kule? Je, kama utaambiwa uache unaweza?

2. TABIA
Kwanza unajenga tabia, baada ya hapo tabia zinakujenga. Mafanikio makubwa sana yanajengwa kwenye msingi mkubwa sana wa tabia. Kila mtu anaweza kuanza hatua ya kwanza. Kila mtu anaweza kuongea, lakini watendaji. Wale wanaoingia uwanjani na kucheza mchezo wenyewe ni wachache sana. Je, umo? Ni rahisi sana kuongea kuliko kutenda.
Baada ya kuona kwamba malengo yanafanya kazi, kitu kingine unachopaswa kufahamu ni kwamba malengo yanaendana na tabia. Katika maisha yako unaweza kujenga tabia yoyote unayoitaka. Wanasaikolojia wanasema kwamba ukirudia kufanya kitu kwa siku 21 mfululizo basi kile kinakuwa sehemu ya maisha yako. Bila shaka ndio maana wahenga wa kizungu walikuja kusema kwamba habit is a second nature. Wakimaanisha “tabia ni asili ya pili”. Kama tabia inaweza kujengwa ndani ya siku 21 basi hii ndio kusema kwamba unaweza kujenga tabia 35 ndani ya miaka 2!!!! What? Ndio tabia 35. Huu ndio muda wako wewe kuanza kujenga tabia. Orodhesha tabia 35 sasa, na anza kuzifanyia kazi moja baada ya nyingine.

Soma Zaidi; TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA-98
TATIZO hujua umuhimu wa nidhamu

3. HAUZUILIKI
Watu walio wengi hawawezi kukusimamisha, mlima mrefu hauwezi kukuzia kuona, MTO mrefu hauwezi kukuzuia kuvuka wewe ndiwe unaweza kujizuia.
Hakuna mtu anayeweza kukuzuia wewe kufanya kitu kikubwa unachotaka. Unaweza kwenda unapotaka na kupata kile unachohitaji. Na ili ufike huko basi unapaswa kufahamu kwamba haupaswi kuishia njiani. Asili ya dunia ipo vizuri sana wala haijawahi kumpendelea mtu. Haiwezi kumpendelea mvivu na kumwacha mchapakazi. Haiwezi kumwinua aliyelala mpaka atakapoamka mwenyewe. Haiwezi kumpandiaha mtu ngazi mpaka apande mwenyewe. Hiyo ndio asili. Kwa hiyo ukifanya vizuri jua kwamba utapokea mazuri sana. Ni asili. Ukikosea itakuadhibu. Mtoto Mdogo hajui kama moto unaunguza, ila akiugusa utamwunguza maana asili iko hivyo.
Maji hayajui kwamba hapa kuna kilima au bonde ila ukiyamwaga yatafuata mkondo tu! Ni asili.
Asili yako pia ni kutozuilika. Unaweza kufika unapotaka, unaweza kupata unachotaka. Unaweza kuwa unavyotaka, hauzuiliki. Kizuizi pekee ni kile unachojiwekea wewe mwenyewe.

Asante sana tukutane kileleni 2018.
Ulikuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391
www.songambeleblog.blogspot.com

Tukutane kesho asubuhi na mapema sana,,,

Jipatie sasa nakala ya TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA na KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI kwa pamoja kwa bei ya sh. 14,000tu badala ya sh. 20,000.

Tuma pesa kwenda nambari 0755848391 jina GODIUS RWEYONGEZA
baada ya hapo nitumie ujumbe wa njia ambayo ungependa nikutumie vitabu hivi, inaweza kuwa wasap, telegram au email.

Karibu sana.

Bei ya kitabu kimoja kimoja

1. TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA (6,000)

2. KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI (8,000).

bei hizi ni kwa siku chache tu baada ya hapo kila kitabu kitakuwa kinapatikana kwa sh. 10,000/-

Ulikuwa nami,
Godius Rweyongeza
($ongambele)
0755848391
www.songambeleblog.blogspot.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X