Katika zama hizi hapa tulizopo kuna vitu ambavyo kuvifanya kwake ni lazima na kuna vitu ambavyo si lazima kuvifanya. Lakini suala hili halijatokea kwenye zama hizi tu. Hata tukirudi kwenye zama za mawe, bado utaona kwamba mababu wetu walikuwa na mbinu za kuhakikisha kwamba wanafanya ili kuhakikisha kwamba wanakuwa wa tofauti. Na vitu hivi hapa si vingine bali vinatokana na kile kitu ambacho mimi hapa nakiita ubunifu. Katika hali ya kawaida kama watu wawili mnazalisha bidhaa ile ile yenye mwonekano ule ule, rangi za bidhaa zile zile na mnauza kwa namna ile ile basi jua kwamba mmoja kati yenu hafai kabisa.
Hii ndio kusema kwamba ubunifu ni jambo ambalo linahitajika kufanyika katika kila sekta. Wala si jammbo la hiari wala si jambo la kusubiri lifanywe na watu wengine. Bali ni jambo ambalo unapaswa kuhakikisha kwamba unalifanya wewe mwenyewe. Ubunifu katika dunia hii sio hiari, ni lazima. Unalazimika kubuni kitu kipya na kuja na mbuinu mpya ya kukutofautisha mwenyewe au utakufa.
Jiulize je kwa nini mimi hapa nina paswa kuwa mbunifu?
Ukipata jibu zuri linalokusuma kubuni kitu usiishie tu hapo bali chukua hatua na kuhakikisha kwamba unaanza kulitumia jibu hilo ambalo wewe hapo umeweza kulipata. Lakini pia hata kama hujapata jibu la msingi sana, mimi niko hapa kukwambia kwamba unapaswa kuhakikisha kwamba unakuwa mbunifu kwa sababu zifuatazo
1. zama zimebasilika maisha yamebasilika ajira sasa zi hatarini basi a wewe unapaswa kuhakikisha kwamba unabadilika. Hakuna jinsi ambavyo unaweza kujihakikishia kuendelea kkubaki kwa namna ile ile katika dunia hii ambay imebasilika kwa kiwango cha hali ya juu sana. Hii ndio kusema kwamba huwezi kwenda kutumia mbinu za mauzo zile zile za jana, lazi,a uwe tayari kujitfautisha wewe hapo mwenyewe na watu wengine. Huwezi kupata matokeo ya tofauti kwa kuendelea kufanya vitu kwa namna ile ile ya kila siku. Hii ndio kusema kwamba lazima uwe tayari kujiotpfautisha wewe hapo na watu wengine. Lakini pia lazima uwe tayati kuibuka na kitu kipya zaidi ya kile ambacho kimezoeleka,
2. vitu vyote haviwezi kufanyika kwa namna moja ile ile kila siku. Katika dunia hii hakuna hata wapishi wawili ambao wanapika chakula kwa namna ile ile kila siku, chakula kile kile, radha ile ile. Kila mpishi anajitahidi kubadillika na kuja kitu chake cha tofauti. Hii ndio kusema kwamba kila mpishi ni wa tofauti na anahakaikisha kwamba amefanya vitu vya tofauti. Kama supu tu iliyopikwa na wapishi wawili ni ya tofauti. Kwa nini wewe hapo ujitahidi kuhakikisha kwamba unakuwa kama ambavyo kila mtu anakuwa akifanya kazi hakikisha kwamba unajitofautisha siku zote na kuja kitu kipya cha kibunifu. Lengo langu ni kuhakikisha kwamba haufanyi kama ambavyo Asha anafanya kilal siku, wala haufanyi kama ambavyo Juma alikuwa anafanya. Wala usiajnze kusema kwamba hapa lazima nifanye kama ambavyo baba yangu alikuwa anafanya zamani zile. Nooo! Zama zimebadika sana, lazima ujiweke katika hali ya kubadilika na kufanyoa vitu vya tofauti ili uweze kuongeza thamani
Hata watu wanaouza chumvi kuna namna wanabuni na kuhakikiisha kwamba chumvi A sio sawa na chumvi B. hii ndio kusema kwamba vionjo, mwonekano wa juu wa chumvi na vitu vingine Zaidi vimekaa kibunifu Zaidi.
Basi akila mara angalila kila kitu katika namna ammbayo wewe hapo unapaswa kukibadillisha na kukiongezea ubunifu wa namna Fulani. Usiache kitu kama amavyo kilikuwa jana. Usisanye kwa namna ambayo kila mtu alifanya jana. Hakikisha kwamba unakuwa wa tofauti kwani wewe ni wa tofauti na vitu vyako lazima view na ubunifu wa tofauti. Ndio kaongeze thamni ya vitu kwa kuvifanyia mchakato wa kibunifu,
Ulikkuwa name
GODIUS RWEYONGEZA
$ongambele
0755848391
JIPATIE VITABU VYANGU VYOTE VIWILI KWA 14,000/- tu. Lipia kupitia nambari 0755848391 jina GODIUS RWEYONGEZA.
Bei ya kitabu kkimoja kimoja,
TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA ni tsh. 6,000/-
KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENNI ni tsh 8,000/-
Wewe ni zaioidi ya ulivyo sasa. Wewe ni mkubwa Zaidi ya ulivyo sasa.
Tukutane kileleni
GODIUS RWEYONGEZA