TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA-95 tatizo unasubiri mwaka mpya


!

Habari ya siku ya leo rafiki yangu! Leo ni tarehe mosi januari 2018! Hongera sana kwa siku hii njema sana ya leo!

Lakini swali langu kwako kitu gani kimebadilika leo!
Nikiangalia nje ya nyumba sasa hivi naona mwanga wa jua kama ilivyokuwa jana. Ninaona ndege wakiruka, lakini hata jana walifanya hivyo. Miti naiona ikimeremeta, ingawa na jana ilikuwa ikimeremeta.

Sasa kitu gani kimebadilika??
kila kitu kitabaki jinsi kilivyo ndani ya mwaka mpya mpaka pale mtu mwenyewe atakapobadilika (songambele’s law of new year). 😁😁😁usishangae. Kama jana ulihairisha kufanya, na leo utahairisha! Huwezi kuniambia nilikuwa nimesubiria mwaka mpya nianze. Motisha ya januari mosi huwa haidumu kama wewe hujabadilika. Baruti zinazopigwa, mbwembwe za kushangilia, nderemo na vifijo ni vya muda tu! Lakini ukibadilika wewe basi utakuwa umebadili maisha yako yote!

Badilika sasa, anza kufanya, kutenda na kuishi kile unachopaswa kuishi.

Lakini hata kama ulikuwa umesubiri mwaka mpya sio vibaya. Ndio huo umefika. Yaani kiufupi leo ndio siku ambayo kwa siku nyingi sana umekuwa ukiisubir! Anza sasa kutimiza malengo yako!

Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio 2018!!
Tukutane kileleni 2018!

Siku njema!

Ndimi
Godius Rweyongeza
($ongambele)
0765848391

KITABU CHA TATIZO SI RASILIMALI KI TAYARI KWA LEO HII UNAWEZA KUKIPATA KWA SHILINGI 5000 TU. HII NI ZAWADI KWA WATU 30 TU NA ZIMEBAKI NAFASI 5 TU! CHUKUA HATUA SASA!


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X