TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA-96 hujaondoa vitu ambavyo sio wewe


Kuna vitu vingi sana ambavyo unafanya ila sio sehemu ya maisha yako na vinapokupeleka sio kule unapopaswa kwenda. Kama utaendelea kuvibeba 2018 basi jua kwamba utakwama, utakwama, utakwama sana. Yaani kuna hatari ya kupita tu 2018.

Je, unavijua vitu ambavyo si wewe? Je, unajua vitu gani ambavyo haupaswi kutembe navyo 2018?

Hii hapa ni orodha kamili ya vitu ambavyo haupaswi kutembea navyo 2018.
1.hofu
2. Uwoga
3. Kuhairisha
4. Uvivu
5. Kutomaliza unachoanza
6. Kutosoma vitabu
8. Kutembea bila Malengo
9. Kuishi maisha ya wengine
10. Imani potofu juu yako

Soma Zaidi; TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA-56 tatizo unawakasirikia watu

Kiukweli hivi vitu sio wewe, na wewe sio hivi vitu. Amua sasa kutembea ndani ya 2018 kama wewe.
Chukua hatua ndogo ndogo kila siku, inawezekana umekuwa unafanya hivi kwa siku nyingi. Yaani kwa siku nyingi umekuwa hutembei wewe kama wewe. Sasa anza kuacha kimoja kimoja. Huwezi kuviacha vyote kwa wakati mmoja. Ila unaweza kuviacha taratibu na mwisho wa siku ukajikuta umejenga tabia nyingine mpya kabisa.

Tabia hazijengwi kwa siku moja,
Mafanikio makubwa hayajengwi kwa siku moja
Bali yanajengwa kwenye msingi wa kufanya kidogo kidogo kila siku.
Mafanikio ya siku moja kwa siku 365 ni sawa na mafanikio ya mwaka mzima.

Kachukue hatua sasa, maana wewe ni zaidi ya ulivyo sasa.

Wewe Ni Zaidi ya ulivyo sasa.
Kujiunga na kundi la wasp la HAZINA YETU BONYEZA HAPA
Ndimi
Coach Godius Rweyongeza
godiusrweyongeza1@gmail.com
www.songambeleblog.blogspot.com
Ili kupata kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI  tuwasiliane kupitia 0755848391

Bonyeza hapa ili uweze kupata makala maalumu kila wiki.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X