TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA-97 tatizo unaogopa vitu vitakavyokufanya ukue


Kuna vitu vingi sana ambavyo vimekuzunguka na vipo kwa ajili yakukufanya wewe ukue.
Watu waliokuzunguka wapo kwa ajili ya kukufanya wewe ukue, japokuwa wanaweza kuwa wanafanya kitu ambacho wewe hupendezwi nacho.
Acha waendelee kufanya kile wanachopaswa kufanya. Wakati wewe ukiendelea na shughuli zako. Inawezekana wana kitu ndani yao wanafanya ambacho wanafanya japo hakikupendezi, ila ni kitu bora sana na kitakufanya ukue. Hakuna aliyejua kwamba Kwa mchezo Bill Gate aliokuwa anaufanya kwa kutumia tarakishishi ungewafanya watu wakue na baadae wajulikane dunia nzima.

Wala hakuna aliyejua kwamba maisha ya yangerahisishwa kwa kuwepo kwa simu na kuwezesha watu kutoka kila kona ya dunia kuwasiliana ndani ya muda kidogo.

Bila shaka aliyetengeneza simu alikuwa anaonekana anafanya kitu kinachohudhi kipindi kipindi kile. Kitu ambacho hata labda wazazi na ndugu zake hawakupenda hata kidogo. Waliogopa kwamba mpendwa wao alikuwa akipoteza muda.
Ila mwisho wa siku alikuja kuwa mtu mwenye umuhimu mkubwa sana,
kumbe
Unapowaona watu wakifanya kazi nyingine, usiogope wape muda mwisho wa siku utaona matokeo makubwa kutoka hapo.

KUMBUKA,
1. . Usikikimbie kitu ambacho kitakufanya ukue
2. Usikatishe watu tamaa kufanya kile kitakachowafanya wakue.
3. Kuanya kitu kitakachokufanya  ukue (na kuwafanya wengine wakue pia) hata kama watu waliokuzunguka wanakiona hakina maana.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
($ongambele)
0755848391

Jipatie Kitabu cha TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA-volume-1 kwa sh. 5000/- tu
Zimebaki nafasi 3 tu!
Chukua hatua muda ndio sasa


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X