Nidhamu katika kazi zetu za kila siku ni jambo la muhimu sana. Nidhamu inaweza kukujenga kama utaitumia vizuri.
Ukosefu wa nidhamu unaweza kukubomoa na kukushusha chini.
Katika kila kitu ufanyacho kila siku weka nidhamu.
Hakikisha unafanya kazi kwa usahihi na kwa ubora hata kama hakuna anayekuangalia. Kama unasubiri umati wa watu ndio ufanye jambo jema sana na la kupendeza, basi jua kwamba ni kosa. Fanya kitu muda wowote hata pale utakapokuwa huonekani mbele ya macho ya watu.
Siku zote gharama unayoitumia kujenga nidhamu ya kazi ni ndogo sana kulinganisha na maumivu ya kuacha kufanya🤔🤔🤔
Kumbe jenga, jenga, jenga nidhamu.
Ndimi,
Godius Rweyongeza
($ongambele)
0755848391
www.songambeleblog.blogspot.com
jipatie vitabu vyangu viwili kwa bei rahisi sana,
Yaani kwa shilingi 14,000/- badala ya 20000/-
😁😁hii inaitwa ya kwako tu!!!
Lipa pesa kwenda nambari 0755848391.,
Gharama hii ya vitabu itadumu kwa kipindi cha muda kidogo sana.
Kama unahitaji Kitabu kimoja kimoja bei yake iko hivi
1. KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI 8000/-
2. TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA(volume-1)
6,000/-
Hii inaitwa ya kwako tu!
Siku njema sana.